Header Ads

Responsive Ads Here

MAHUSIANO SIO MABAYA ILA TUNAHUSIANAVIBAYA

Leo tena Elias Patrick a.ka ellysbrand ameeleza kwa kina vitu vya kuzingatia katika mahusiano . Ambavyo wengi wamevipuuzia lakini vimefanya watu wayachukie sana mahusiano . Anaanza kwa kusema . Mahusiano sio mabaya tatizo ni tunahusiana Vibaya .

Maswala ya mahusiano haijalishi ni ya kinamna gani, iwe ya kitaaluma, ya kirafiki, ya kimapenzi, ya kindugu, ya mume na mke, ya mzazi na watoto, ya kikazi, ya kibiashara, mahusiano ya aina mbali mbali katika jamii, yana changamoto zake na kwa sababu ya uwingi wa changamoto katika hayo mahusiano kuna namna sahihi ya kuenenda katika hayo.
Namna unavyohandle changamoto mbali mbali katika mahusiano itaamua mafanikio yako au kukwama kwako katika maswala mazima ya mahusiano.
Mahusiano yanahitaji sana kuchukuliana, kuelewana, kuvumiliana, kusameheana.Tupo tofauti sana na kile ambacho ni sawa kwa mmoja kinaweza kisiwe sawa kwa mwingine. Mashindano, kujiona bora, kutokumzingatia mwingine na hisia zake kunaweza kutufanya tufeli sana katika maswala mazima ya mahusiano.
Jitahidi kutafuta kuelewa wengine na misimamo yao na mitazamo yao alafu chukuliana nao hivyo hivyo.
Kuthibitisha kuwa wewe upo sawa au mwingine amekosea sio vitu ambavyo vinasaidia sana kujenga mahusiano.
Kuna mambo mengine unayaacha tu.
Heshimu haki ya mtu mwingine kuwa na mtazamo wake, namna yake anavyoona na sio kila wakati mtazamo wake au namna anavyoona kukawa sahihi kwa muono wako.
Sio lazima kila wakati uwe sahihi na hata ukiwa sahihi sio lazima utumie nguvu kubwa sana kuthibitisha wewe upo sahihi na mwingine hayupo sahihi.
Yaani unaweza tu ukatoa mtazamo wako, wazo lako, unavyojua wewe na ukaacha muda uamue kama upo sahihi au la.
Kukosea kimtazamo haijawahi kuwa kosa la jinai maana kila mmoja wetu alishawahi kukosea kimtazamo na tutaendelea kukosea kimtazamo maana kila siku twajifunza.
Kudhabihu mahusiano kwenye madhabahu ya wewe haupo sahihi, kilicho sahihi ni hiki wakati mhusika akiachwa atakuja tu kukua katika mtazamo wake na ufahamu wake na hatimaye kubadilika ni kutokuthamini mahusiano hata kidogo.
Sema ule ukweli unaoujua, sema ule ufahamu unaoujua alafu acha muda uuthibitishe huku kwa kadiri iwezekanavyo ukilinda mahusiano yako na wengine.
Kununiana, kuchuniana, kusemeshana mbovu au kwa mafumbo iwe ni live au kwa mawasiliano ya kielektroniki sio namna sahihi sana ya kuhusiana.
Watu wanakosea aise kama sisi tu tunavyokoseaga.
Ila pia watu wanakua na kubadilika ...../

Naamini nimeongea na Mtu . Mungu wa mbinguni akupe amani, furaha na hekima ya kuishi huku ukilinda moyo wako usiumizwe kwani ndio wenye dhamana ya kupenda ukiumizwa ndo basii unaanza kuwa mtumwa wa furaha yako mwenyewe
Imeandikwa na Elias Patrick ( Ellys Brand )
Instagram : ellys_brand
Kupata post za @ellys_brand kwa njia ya what's app tuma jina lako kwenda namba 0737490115*

No comments