Header Ads

Responsive Ads Here

MSD YAPELEKA DAWA GEREZANI WILAYANI NGARA MKOANI KAGERA

 Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Mwanza, Cornelia Mwillawi  (katikati), akiwakabidhi dawa na mifuko yenye vifaa vya kujifungulia wajawazito (Delivery Pack) wajumbe wa kamati ya afya  wa Jeshi la Magereza wa Gereza la Mifugo la Rusumo wilayani Ngara mkoani Kagera jana. Kutoka kulia ni Koplo Apelius Kamugisha, Sajeni Scolastica Saganda na Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya gereza hilo, Koplo Hashimu Bilalamo.
 Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya gereza hilo, Koplo Hashimu Bilalamo.
 Makabidhiano ya dawa yakiendelea.
 Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya gereza hilo, Koplo Hashimu Bilalamo (kulia), akisaini fomu maalumu baada ya kupokea dawa hizo. Kutoka kushoto ni Mfamasia wa Wilaya ya Ngara, Patrick Ago, Afisa Huduma kwa Wateja wa MSD Kanda ya Mwanza, Cornelia  Mwillawi na  mjumbe wa kamati ya afya wa Gereza hilo, Koplo Scolastica Saganda. Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Mwanza, Cornelia Mwillawi  (kulia), akiwakabidhi mifuko yenye vifaa vya kujifungulia wajawazito (Delivery Pack) wajumbe wa kamati ya afya  wa Zahanati ya Rusumo ambapo pia walikabidhiwa na dawa za aina mbalimbali. Kutoka kushoto ni Muuguzi wa zahanati hiyo, Lydia Samuel, Mganga Mfawidhi, Flavian Joseph na Mwenyekiti wa Kamati ya Afya wa Zahanati ya Rusumo, Emanuel Living.
 Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Rusumo, Flavian Joseph na Mwenyekiti wa kamati ya afya wa zahanati hiyo, Emanuel Living wakiingiza dawa kwenye mtumbwi katika kivuko cha mto Luvuvu kwa ajili ya kuzipeleka katika zahanati hiyo. Jengo la Zahanati ya Kabanga iliyopo karibu na mpaka wa Burundi na Tanzania.
 Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Mwanza, Cornelia Mwillawi (kulia), akiwakabidhi dawa wafanyakazi wa Zahanati ya Kabanga. Kutoka kushoto ni Daktari wa zahanati hiyo, Abas Mwoseka, Muuguzi wa Zahanati hiyo, Esteria Julius na Mganga Mfawidhi, Juventh John.

Na Dotto Mwaibale, Ngara Kagera

Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Gereza la Mifugo lililopo wilayani Ngara mkoani Kagera, Koplo Hashimu Bilalamo ameipongeza Bohari ya Dawa (MSD) kwa mpango wa 
kuwapelekea dawa wateja wake katika vituo vyao.

Bilalamo alitoa pongezi hizo jana kwa waandishi wa habari ambao wapo ziarani mkoani Kagera kuangalia taratibu za usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwenye vituo vya kutolea huduma za afya mkoani Kagera zinazo fanywa na MSD.

"Tunapenda kuipongeza MSD kwa mpango wake wa kuwapelekea dawa wateja wake kwenye vituo vyao kwani unasaidia sana" alisema Bilalamo.

Alisema katika zahanati hiyo dawa zote muhimu wanazipata kwa wakati na kuwa wagonjwa wanaopata huduma za afya ni watu wafungwa wanaotumikia adhabu zao katika gereza hilo, familia za askari na jamii inayoishi jirani na gereza hilo.

Afisa Huduma kwa Wateja wa MSD Kanda ya Mwanza, Cornelia Mwillawi alisema MSD imekuwa na utaratibu wa kuwafikishia vifaa tiba na vitendanishi vya maabara wateja wao kote nchini.

"Ni utaratibu wetu wa kuwafikishia wateja dawa hadi kwenye vituo vyao ili kuhakikisha kila mwananchi anapata dawa kwa wakati" alisema Mwillawi.

Alisema ili kuongeza nguvu ya upelekaji dawa nchini kote serikali kupitia mfuko wa fedha wa pamoja (Global Fund) mapema mwaka huu ulitoa magari 180 kwa MSD kwa ajili ya kazi hiyo ambayo yamesambazwa nchi nzima.

Katika ziara hiyo wilayani humo, MSD Kanda ya Muleba imeweza kukabidhi dawa katika zahanati za gereza hilo, Kabanga na Rusumo. 

No comments