Header Ads

Responsive Ads Here

MSD MULEBA YAPELEKA HUDUMA ZAKE MKOANI GEITA

Kaimu Meneja wa Mauzo wa Kituo cha Wilaya ya Muleba, Wasante  Nyihirani, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu shughuli zinazofanywa na MSD Kituo cha Muleba.
Magari ya usambazi dawa ya MSD yakiwa nje ya kituo hicho.
Jengo la Utawala la Kituo cha Mauzo cha MSD Wilaya ya Muleba.
Ghara la kuhifadhi dawa Kituo cha Mauzo MSD wilayani Muleba


Na Dotto Mwaibale, Muleba

BOHARI ya Dawa (MSD) Kituo cha Muleba  kimesogeza huduma zake za usambazaji dawa mkoani Geita ili kuwapunguzia safari ndefu ya kwenda kupata huduma hiyo Kanda ya Mwanza.

Hayo yalibainishwa jana na Kaimu Meneja wa Mauzo wa Kituo cha Wilaya ya Muleba, Wasante  Nyihirani wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao wapo ziarani mkoani Kagera kuangalia taratibu za usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwenye vituo vua kutolea huduma za afya mkoani Kagera.

"Zamani mkoa wa Geita ulikuwa ukipokea dawa kutoka Kanda ya Mwanza lakini wadau wengine na serikali ikiona ni vema kuwasogezea huduma karibu ili kuwapunguzia gharama za usafiri na kupata dawa kwa wakati" alisema Nyihirani.

Alisema katika mkoa huo wilaya zilizonufaika na uanzishwaji wa kupeleka dawa mkoani Geita ni Wilaya ya Mbogwe DC na Bukombe DC ambazo nazo zimekuwa zikitoa huduma katika maeneo mengine ya mkoa huo.

Alisema kuanzishwa kwa kituo cha mauzo cha Muleba kumewapunguzia mzigo Kanda ya Mwanza ambayo ilielemewa kwa vile ilikuwa ikihudumia mikoa  ya Kagera na Geita.

Alisema kituo hicho cha Muleba hivi sasa kinatumia majengo ya Halmshauri ya wilaya hiyo ambayo yalikuwa yakitumika kama hospitali na kuwa MSD iliyafanyia ukarabati mkubwa kulingana na mahitaji yao.

Alisema katika majengo hayo wametenga eneo la kuhifadhia dawa baada ya kuzipokea, eneo la kuhifadhi dawa za kawaida, zilizokwisha muda wake, usambazaji kabla ya kwenda kwa mteja na eneo la kuhifadhia dawa zinazo hitaji baridi.

Nyihirani aliongeza kusema kuwa kituo hicho cha Muleba kina hudumia wilaya 10 nane zikiwa za mkoa wa Kagera na mbili za mkoani Geita.

No comments