Header Ads

Responsive Ads Here

UBA BENKI TANZANIA YAJIDHATITI ZAIDI KUWAHUDUMIA WATEJA WAKE NA KUWAINUA KIUCHUMI


(KUSHOTO)MKUU wa Idara ya Mahusiano ya Kimataifa wa UBA Nasir Ramon, Katikati ni Toruka Osadukwa Meneja bidhaa wa UBA na kulia ni Brendasia Kileo Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa UBA wakiongea na waandishi wa habari hawapo pichani katika hoteli ya Golden Tulip iliyopo Posta Jijini Dar es Salaam.
****
UONGOZI wa United Bank Of Africa(UBA)umesema umejipanga kuendelea kutoa huduma bora za kifedha kwa Watanzania huku ukisisitiza kukua kwa teknolojia kumeifanya benki yao kutoa huduma zake kwa njia ya mtandao na kuwafikia wateja wengi zaidi.
Pia umeeleza mikakati yao katika kuhakikisha wanashiriki katika kuleta maendeleo nchini na kuahidi kuendelea kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Tano  kuleta maendeleo ya wananchi.
Pamoja na hayo uongozi huo umewahimiza wananchi umuhimu wa kuwa na Kitambulisho cha Taifa kwani ni muhimu na kufafanua wenye vitambulisho hivyo inakuwa rahisi kupata huduma za kifedha kwenye benki yao kwani husaidia kupata taarifa zote muhimu za mteja.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na uongozi wa UBA wakati wanazungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusu mafanikio, malengo na mikakati yao katika utoaji wa huduma za kibenki nchini.
Mtendaji Mkuu wa UBA nchini Tanzania Chris Byaruhanga ,amesema tangu kuanzishwa kwa benki hiyo miaka 75 iliyopita nchini Nigeria na kufungua matawi katika nchini mbalimbali ikiwemo Tanzania wamepata mafanikio makubwa na benki hiyo imekuwa chachu ya maendeleo kwa Bara la Afrika.
Amefafanua kwa Tanzania UBA imeendelea kujiimarisha katika kutoa huduma bora za kibenki ambapo pia imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia shughuli za kimaendeleo na kubwa zaidi uwepo wa benki hiyo mesaidia katika kutoa ajira kwa Watanzania.
"Hivi karibuni tunatarajia kwenda kufungua tawi Mjini Dodoma kwani tunatambua kuwa Makao Makuu ya Serikali yamehamia huko nasi lazima twende huko kwa ajili ya kuwahudumia wananchi.Hivyo tawi hilo litakapofunguliwa litahitaji watu wa kuwaajiri ambao nao watakuwa Watanzania,"amesema.
Pia Byaruhanga amefafanua licha ya kutoa huduma zao kwa njia ya mtandao zaidi bado wameendelea kushirikiana na benki ya CRDB kwa ajili ya kuwafikia wateja waliopo maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuwapa huduma za kifedha.
 "Malengo yetu ni kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuwahudumia wateja wa makundi mbalimbali kulingana na vigezo vyao.
"Tunaamini kuwa mbali na mambo mengine pia itasaidia kukuza uchumi wa Taifa na maendeleo kwa ujumla wake,"amesema Byaruhanga.
Kwa upande wa Mkuu wa Uhusiano ya ndani wa UBA Kanda ya Afrika Nasir Ramon, amesema UBA inayotoa huduma zake katika  nchi 20 za Bara la Afrika, Marekani, Uingereza na Ufaransa.
Amesema UBA ina mtaji wa Dola za Marekani zaidi ya Bilioni 12, na hivyo kujidhatiti katika utoaji wake wa huduma katika nchi yoyote.
Amesema malengo mengine ya benki hiyo nchini ni kuhakikisha inaongeza kwa kuwa na wateja wengi huku akisisitiza usalama wa fedha za wateja wao ni mkubwa.
"Dhamira yetu ni kuona tunaendelea kuwahudumi wananchi wa Bara la Afrika ikiwamo Tanzania kwa kuhakikisha tunashiriki kuleta maendeleo yao na ndilo moja ya jukumu la benki hii tangu kuanzishwa kwake.Ni benki ambayo imesambaa katika nchi nyingi za Afrika,"amesisitiza.
Amehimiza Watanzania kuchangia fursa ambazo zinatolewa na benki hiyo ikiwemo ya utoaji mikopo yenye riba nafuu na kupongeza jitihada za Serikali zinazozungumzia kuwa na benki imara na zenye tija kwa wateja.
Amegusia umuhimu wa kitambulisho cha Taifana kwamba kitambulisho hicho n muhimu hata kwa wale wanaohitaji kufungua akaunti katika benki kwani ni rahisi kupata taarifa muhimu za mteja.
Hivyo ameshauri ipo haja ya kila mmoja kuona thamani ya kuwa na kitambulisho cha taifa.Kwa nchini Nigeria kitambulisho hicho kinatumika maeneo mengi zaidi na lazima raia awe nacho
Wakati huo huo Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo Brendansia Kileo, amewataka wananchi kujitokeza na kujiunga na benki hiyo ili wanufaike na huduma za kifedha wanazotoa na wanachojivunia wao huduma zao zipo kiganjani zaidi kwani kukua kwa teknolojia ya mtandao kumerahisisha utoaji huduma.
Mwisho

No comments