Header Ads

Responsive Ads Here

MZEE MAJUTO AAGWA RASMI

Wasanii wa filamu pamoja na baadhi ya wasanii wa muziki Tanzania, wamemsindikiza na kumuaga muigizaji mwenzao Amri Athumani maarufu kama Mzee Majuto, ambaye anelekea nchini India kwa matibabu.

Akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake muigizaji Hashim Kambi amesema wanamuombea Mzee Majuto asafiri salama na kupata matibabu, ili atakaporudi waendelee kuungana naye kwenye kazi za sanaa.

Sambamba na hilo wasanii hao wameishukuru serikali kupitia waziri wake wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harison Mwakyembe, pamoja na Rais Magufuli kwa mchango wao walio uonyesha kuwasaidia wasanii kwenye matatizo mbali mbali.

"Tunamuombea kila la heri Mwenyezi Mungu amchukue salama, amfikishe salama na apate tiba anayostahili, Mzee Majuto arejee hapa akiwa mzee Majuto tena, tupo na umoja kama wasanii na kubwa sana tunamshukuru waziri wetu ambaye anahusika na tasnia yetu kwa bidii aliyofanya, Mwenyezi Mungu amrehemu, lakini pia shukran za dhati ziende kwa jembe letu hapa ni kazi tu John Magufuli kwa kusaidia wasanii, tumuombee mzee wetu aende salama arudi salama”, amesikika Mzee Kambi.

Mzee Majuto amesafirishwa leo kuelekea nchini India ili kupata matibabu zaidi ya tezi dume, ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.

No comments