Header Ads

Responsive Ads Here

MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA (TPC) ATOA TAARIFA YA UTENDAJI WA TPC KWA KIPINDI CHA MWAKA 2016/2017

Baadhi ya watendaji wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari, wakati Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo alipokuwa akitoa taarifa ya utendaji ya shirika kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017, jijini Dar es Salaam leo.  
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo, wakati akitoa taarifa ya utendaji wa Shirika kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017, jijini Dar es Salaam leo.  
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe, akizungumza wakati akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo (kushoto), ili atoe taarifa ya utendaji ya shirika kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017, jijini Dar es Salaam leo.   
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini wakati Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo, akitoa taarifa ya utendaji wa Shirika kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017, jijini Dar es Salaam leo.  
Baadhi ya watendaji wa Shirika la Posta Tanzania, wakiwa katika mkutano huo na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya watendaji wa shirika la Posta Tanzania, wakiwa pamoja na waandishi wa habari wakinakili taarifa iliyokuwa ikitolewa na Mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo, katika mkutano huo, jijini Dar es Salaam leo.  
Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akitoa taarifa ya utendaji ya shirika kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017. Kulia ni Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Shirika la Posta Tanzania (TPC), Elia Madulesi, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo. 
Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo, akizungumza na waandishi wa habari, wakati akitoa taarifa ya utendaji ya shirika kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017. Katikati ni Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe na kulia ni Kaimu Meneja Uendeshaji Biashara wa shirika hilo, Mwanaisha Saidi
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe, akijibu maswali ya waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Haruni Kondo na kushoto ni Meneja Rasilimali za Shirika wa TPC, Macrice Mbodo.  
Kaimu Meneja Uendeshaji Biashara wa Shirika la Posta, Mwanaisha Saidi (kulia), akijibu badhi ya maswali ya waandishi wa habari katika mkutano huo.  
Meneja Rasilimali za Shirika wa TPC, Macrice Mbodo (kushoto), akijibu badhi ya maswali ya waandishi wa habari na kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali wakati kuhusu shirika hilo, katika mkutano huo. 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe, akiwashukuru waandishi wa habari baada ya Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo (kushoto), kumaliza kutoa taarifa ya utendaji ya shirika kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017, jijini Dar es Salaam leo. 

TAARIFA YA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA KWA WAANDISHI WA HABARI TAREHE 3 MEI, 2018 UKUMBI WA BODI POSTA HOUSE:
NDUGU KAIMU POSTAMASTA MKUU,

MENEJIMENTI YA SHIRIKA LA POSTA,

NDUGU VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI,

NDUGU WANAHABARI, MABIBI NA MABWANA.

Ndugu wanahabari, tumewaita hapa leo tarehe 03/05/2018 ili kuwapa taarifa fupi juu ya utendaji wa Shirika la Posta Tanzania kwa kipindi mwaka wa fedha 2016/2017 tangu mimi na bodi yangu tumeingia kuongoza Shirika la Posta Tanzania.
1. UTANGULIZI
Ndugu wanahabari,

Kama mnavyofahamu tulipoingia kuanza kazi mimi na bodi yangu tulikutana na changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ;

Ø Mapungufu katika kusimamia nidhamu, uadilifu, weledi na upimo wa utendaji, kubadilisha mitizamo ya Wafanyakazi, udhibiti wa mapato na matumizi ya Shirika.

Ø Maslahi duni ya Wafanyakazi, utendaji kazi wa mazoea na kutojali matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA).


Baada ya kuingia tulitaka kujifunza na kuona namna tunavyoweza kuongeza tija na ufanisi kwa kutumia rasilimali zilizopo katika Shirika hii ni pamoja na:

Kuongeza miundombinu ya Shirika la Posta ikiwa ni pamoja na miliki zake na vitendea kazi.

Ø Kuongeza ufanisi wa kiutendaji ili kukuza wingi na ubora wa biashara pamoja na kuhakikisha kunakuwepo faida kwa Shirika na kutoa gawio kwa mwenye mali (Serikali).

Ø Kupanua mtandao na wigo wa soko ili wananchi wote hadi huko vijijini wapate kufikiwa na huduma bora na za kisasa.

Ø Kufuatilia ukasanyaji wa mapato ya Shirika kutoka vyanzo mbalimbali ambavyo havikuwa vikijulikana hasa eneo la miliki za Shirika, kama majengo n.k.

Ili kufanikisha azma hiyo ,Bodi ilichukuwa hatua mbali mbali ikiwa ni pamoja na kutoa miongozo ,maelekezo na kusimamia kwa karibu Shirika ili kuwezesha menejiment kuchukua hatua za kinidhamu kwa wale wote walionekana ni kikwazo cha juhudi hizo.


2. UENDESHAJI WA SHIRIKA:
Ndugu wanahabari,
        A) CHANGAMOTO ZA SHIRIKA:
Ø Pamoja na changamoto zilizokuwepo, sisi kama bodi ya wakurugenzi tuligundua kuwa zipo fursa nyingi tu za kupanua na kuboresha biashara zetu,pia udhaifu katika kukusanya mapato ya Shirika.

Ø Tunao mtandao wetu mpana wa kitaifa wa ofisi zipatazo 400 zilizounganishwa na zaidi ya ofisi 660,000 dunianikwenye zaidi ya nchi 192 wanachama wa Umoja wa Posta Duniani unaowezesha kupanua na kuboresha zaidi biashara zetu ndani na nje nchi kwa minajili ya kukuza mapato.

       B) MABADILIKO YA UONGOZI NA MTAZAMO WA SHIRIKA:
Katika lengo la kuleta tija na ufanisi kwenye Shirika Bodi imefanya mabadiliko mbalimbali ya kiuongozi ili kuliwezesha Shirika kwenda na spidi ya Serikali ya awamu ya tano ya raisi wetu mpendwa Mheshimiwa John  Joseph Pombe Magufuli ya “HAPA KAZI TU”.

Mabadiliko hayo ni pamoja kuondoa viongozi waliokuwepo na kuweka vijana ambao wataweza kufanya kazi kwa Maono na Mwelekeo wa Shirika, Kasi ya utendaji ili kuleta Tija na Ufanisi utakaokidhi matarajio ya Shirika tunayoyataka.
Viongozi tuliowapa nafasi hizo ni vijana na wana ari na nguvu,tunatarajia watafanya kazi zao kwa weledi na tutawapima baada ya muda kuona kama wanakwenda na kasi tunayoitaka.
Viongozi hao tuliowapa nafasi ni pamoja na:
i) Meneja Mkuu /Uendeshaji wa Biashara Bi. Mwanaisha Ali Said
ii)  Meneja wa Barua na Lojistiki Bw. Josephat Gabliel,
iii) Katibu wa Shirika Bw.Erick Maximillian
iv) Meneja wa Masoko Bw.Walter Mariki
v) Meneja Huduma za Kifedha Bi.Rehema Mbunda
vi) Meneja EMS Bi Mariam Malembeka
vii) Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi Bw. Juma Swedi

       C) VITENDEA KAZI NA MASLAHI YA WAFANYAKAZI:
Tulipoingia kwenye uongozi wetu tuligundua kuna shida ya vitendea na mazingira duni ya wafanyakazi ikiwemo mishahara na mazingira yasiyoridhisha ya kazi jambo ambalo limekuwa linarudisha nyuma juhudi za Shirika kusonga mbele.
Ø Tumeongeza vitendea kazi ikiwemo magari na pikipiki ili kurahisisha usafirishaji wa barua ,vifushi na vipeto.

Ø Tumeweka Scanner mpya ili kulinda usalama wa mali za wateja na ufuatiliaji wa bidhaa haramu kupita kwenye mfumo wa Posta.

Ø Tunatambua kuwa maslahi ya wafanyakazi wetu siyo ya kiwango cha kuridhisha na ndiyo maana mimi na bodi yangu tunapigania maslahi bora kwa wafanyakazi nyanayozingatia ongezeko la ufanisi na tija. Tumejiweke lengo baada ya muda katika kipindi hiki kabla ya mwisho wa mwaka huu wa fedha tutakuwa tumefanya maboresho ya maslahi ya wafanyakazi wetu

D) MATUMIZI YA TEHAMA:
Bodi yetu inasisitiza sana matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika utendaji kazi. Hii ndiyo sababu tunawekeza fedha nyingi katika mifumo ya TEHAMA, Shirika linatumia karibu milioni 224 (hii ikijumuisha Net smart, Utrack, IPS, IFS na Paymaster)  kwa ajili ya mifumo kwa mwaka katika kuhudumia ofisi zaidi ya ofisi 120 zilizounganishwa nchini kote na zaidi ya compyuta 1000 . Kwa sababu hiyo hatuna mchezo na mfanyazi asitaka kutumia mifumo.
Tunafahamu wengine hawataki uli kuhujumu na kuvuruga mifumo ili wafanye uhalifu wao, hatua kali za kinidhamu zimechukuliwa na zitaendelea kuchukuliwa ili kujenga Poista mpya yenye hadhi na inayoaminika.  
Ø Matumizi mazuri ya TEHAMA yamewezesha kuanzisha biashara mpya za kimtandao kama vile e-Philately na huduma jumuishi mahali pamoja (Unified Community Services) au Huduma Express.

Ø Tumeongeza idadi ya ofisi za Posta zilizounganishwa kwenye mtandao kutoka 105 hadi 120 zimeunganishwa kwenye mtandao wa TTCL na lengo ni kufiki ofisi 135 ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni,2018.

Ø Tumeweka mifumo ya kufuatilia magari ya Shirika (Car Track total control)yanayobeba barua na mali za wateja ili kuongeza usalama na matumizi mazuri ya magari na mafuta.

Ø Ushindani umekuwa fursa nzuri kwetu hatuuangalii hilo kama changamoto pekee lakini kwa upande mwingine imekuwa fursa nzuri ambayo imetuwezesha kuboresha, kupanua na kubuni huduma mpya zinazohitajiwa na soko na wateja wetu kwa sasa.

E) MIKATABA YA KIBIASHARA:

Ili kuongeza mapato ya Shirika na kuweza kulipa gawio kwa mwenye mali ambaye ni Serikali, Bodi kwa kushikiana na menejimenti imeweza kuingia mikataba zaidi 94 ya kibiashara na taasisi mbalimbali za Serikali ,binafsi na taasisi zisizo za kiserikali katiak kipindi cha Januari hadi Mei,2018.

Tunatumia nafasi hii kuomba taasisi zote za Umma kuitumia huduma za Posta maana ndiyo chombo pekee cha Serikali kilichopewa jukumu la msingi la kufanya huduma za kiposta. Pia ikumbukwe kuwa Sheria iliyonda Shirika la Posta mwaka 1993 iliyoanza kazi rasmi mwaka 1994 , kifungu cha 8d.

F) POSTA MLANGONI:
Katika kuwahudumia wateja wetu kwa kadri ya mahitaji yao tulianzisha huduma ya Posta Mlangoni ikiwa na lengo la kuwafikia wateja pale walipo. Tunashukuru huduma hii imepokelewa vema na wateja na inaendelea vizuri.

Kuna changamoto katika mfumo wa utoaji huduma hii hasa tunawaomba wenzetu wanaoshugulikia uenedelezaji wa anuani za makazi kuongeza kasi ya kuweka majina ya mitaa na namba za nyumba ili kutuwezesha kufikisha huduma kwa wateja wetu kwa urahisi. Nitoe rai yangu kwa wahusika kutusaidia katika hilo.

3. MAFANIKIO YA BODI
Ndugu wanahabari,
Napenda kuwajulisha kuwa katika kipindi hiki kifupi kwa ushirikiano uliopo kati ya bodi na menejimenti kumekuwa na mengi yamefanyika kati hayo machache ni:
Ø Tumeongeza uwajibikaji kwa watumishi wa kada zote ndani ya Shirika kwa kujenga nidhamu ya kazi, kujituma, kuheshimu kanuni na taratibu, kuongeza ubunifu na kufanya kazi kwa ufanisi wenye tija.

Ø Tumebadilisha mitazamo (mind sets) ya wafanyakazi wetu ili tuondokane na kuendesha shughuli kwa mazoea yaani “business as usual”.

a) Miliki za shirika:
Kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu bodi iteuliwe kwa kushirikiana na menejimenti na watendaji wake shirika limeweza kuweka kumbukumbu sahihi za  viwanja vya shirika zipatavyo 198,ambazo kati ya hizo hati 161 vimeendelezwa.

b) Kurejeshewa madeni ya pensheni:
Baada ya juhudi za bodi na menejimenti kufanyika serikali imeridhia kurudisha madeni ambayo Shirika linaidai serikali ya karibu shilingi bilion 3.9 ambayo ni deni la pensheni za wastaafu wa lililokuwa Shirika la Posta na simu la Afrika Mashariki zinazolipwa na Shirika kwa niaba ya Serikali kwa kipindi kilichishi juni 2016.
Hadi mwezi machi mwaka huu 2018 deni limefikia Tshs.bilioni 4.7

Fedha hizi ni za utendaji na zikipatikana zitawezesha kuongeza mtaji wetu na kuboresha vitendea kazi na hivyo kuongeza tija na faida kwa Serikali ambaye ndiyo mwenye mali.

c) Payment Switch
Mikakati mingine iliyofanywa na bodi na menejimenti kwa katika kipindi hicho ililenga katika kuboresha huduma na biashara zetu, kwa mfano sasa hivi Shirika lipo kwenye mpango wa kununua payment switch ifikapo mwezi wa Julai, hii itaongeza ufanisi katika kufanya biashara mtandao na pia kuwezesha biashara mpya za kimtandao


KWA KUMALIZIA:

Ndugu wanahabari,

Napenda kutoa taarifa kuwa uongozi wetu pamoja na haya yote niliyoeleza, Shirika kwa mara ya kwanza katika kipindi hiki mbali na changamoto mbalimbali zikiwemo za kurithi , kama mnavyojua hili ni Shirka kongwe tumepata mafaniko kupitia hatua mbalimbali tulizozichukua, zingine zilikuwa ni ngumu na zingine za kimaelekezo, mpaka sasa kuna mwelekeo unaoanza kuonekana kwa utendaji wa shirika hili.

Katika kipindi cha mwaka:

 2015/2016 Shirika lilipata hasara ya Tshs. 3,490,031,800/=

 2016/2017 Shirika limeweza kupata faida ya Tshs.1,014,548,869/=  baada ya kodi

Kwa kipindi cha Julai hadi Disemba 2017 Shirika limepata faida ya Tshs. 1,375,797,632/= baada ya kodi

Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru sana wateja , wadau wetu wote mkiwemo nyinyi wanahabari na umma kwa ujumla kwa kutuunga mkono katika juhudi za kuwatumikia wananchi wetu.
Asanten sana kwa kunisikiliza na Mungu awabariki sana.


Imetolewa na:

Lt. Kanali Mstaafu, Dr.Haruni Kondo,

Mwenyekiti, Bodi ya wakurugenzi
Shirika la Posta Tanzania
No comments