Header Ads

Responsive Ads Here

MPINA AMWAGA PIKIPIKI KWENYE MINADA YA MIPAKANI


  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina(mwenye
miwani) akikagua moja  kati ya  pikipiki kumi kabla ya kuzikabidhi
ili zitumike kwenye minada ya mipakani na upili.Picha na John Mapepele
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina (mwenye
miwani) akikata utepe kwenye moja  kati ya  pikipiki kumi
kabla ya kuzikabidhi ili zitumike kwenye minada ya mipakani na upili.Picha
na John Mapepele
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina (mwenye
miwani) akienesha  moja  kati ya  pikipiki kumi baada
ya kuzikabidhi ili zitumike kwenye minada ya mipakani na upili.Picha
na John Mapepele
Asema zitasaidia kukomesha utoroshaji wa mifugo nje
ya nchi
 Na John Mapepele
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ameagiza maeneo yote ya minada ya
awali na upili yapimwe na kuwekwa alama za mipaka katika mwaka wa fedha
2018/19 ili kuepuka uvamizi unaofanywa na watumiaji wengine wa ardhi.
Maelekezo
hayo ameyatoa leo kwenye hafla ya iliyofanyika kwenye Ofisi ya Dar es
Salaam wakati akikabidhi pikipiki kumi ili zitumike kwenye mipaka na
minada ya upili kwa lengo la kudhibiti utoroshaji wa mifugo na mazao
yake nje ya nchi.
Alisema Serikali inakusudia kuifunga minada
yote iliyoanzishwa kiholela kwa nia ovu ambapo amesema kuendelea kubaki
kwa minada hiyo kunadhoofisha minada ambayo imeanzishwa kwa kufuata
taratibu za Serikali.
Aidha, Waziri Mpina alisema kuanzia sasa
minada yote itaboreshwa na kuwa katika mfumo wa kielektroniki ili
kudhibiti mapato ya Serikali kwa njia za kisasa zaidi.
“Kuanzia
sasa wizara yangu inaingia kwenye mfumo mpya katika kusimamia minada
yote ambapo utaiunganisha kwenye mfumo wa kielektroniki” alisisitiza
Mpina
Sambamba na hatua hiyo Mpina amemwagiza Katibu Mkuu
anayeshughulikia Sekta ya mifugo Dkt. Mary Mashingo kuhakikisha miundo
mbinu ya minada yote inakarabatiwa mara moja na ili kuboresha usimamizi
wa sekta ya mifugo nchini.
Alisema Wizara inasimamia minada 12
ya upili na 10 ya mipakani ambapo minada ya upili ipo nchi nzima kwa
kuzingatia wingi wa mifugo katika eneo husika.
Mpina alisema
hapa nchini kuna minada 465 ya awali ambayo huendeshwa na Mamlaka za
Serikali za Mitaa (MSM). Aidha, minada ya mipakani imewekwa kuzingatia
njia za kusafirishia mifugo kwenda nje ya nchi.
Alitaja minada
ya upili na Wilaya ilipo kuwa ni Pugu (Ilala), Kizota (Dodoma), Sekenke
(Iramba), Igunga (Igunga), Ipuli (Tabora) na Mhunze (Kishapu). Mingine
ni Nyamatala (Misungwi), Meserani (Monduli), Themi (Arumeru), Weruweru
(Hai), Korogwe (Korogwe) na Lumecha (Songea). Aidha, minada ya mipakani
ni pamoja na Buhigwe (Kasulu), Kasesya (Kalambo), Kileo (Mwanga), Kirumi
(Butiama), Longido (Longido) na Waso (Ngorongoro).
Minada
mingine ni Mpemba (Momba), Kakonko (Kakonko), Mtukula (Misenyi) na
Rusumo (Ngara). Minada itakayokabidhiwa pikipiki hizi ni Muhunze,
Sekenke, Ipuli, Korogwe, Weruweru, Lumecha, Kasesya, Murusagamba,
Buhigwe na Kirumi.
Aliongeza kuwa lengo la kuwepo kwa minada ya
mifugo katika maeneo mbalimbali nchini ni kutoa fursa kwa wafugaji na
wafanyabishara ya mifugo kuuza mifugo yao kwa faida zaidi kwa kuzingatia
ushindani wa soko.
Naye katibu Mkuu Dkt. Mashingo alimshukuru
Waziri kwa kuzindua matumizi ya pikipiki hizo na kuahidi kwamba pikipiki
hizo zitaleta ufanisi katika utendaji kazi wa minada hapa nchini.
Alisema
Tanzania inakadiriwa kuwa na ng’ombe millioni 30.5, Mbuzi millioni
18.8, na Kondoo millioni 5.7. Aidha, Katika mwaka 2017/18 jumla ya
ng’ombe 1,614,321, Mbuzi 1,340,222 na Kondoo 315,636 wenye thamani ya
shilingi trillioni 1.1 waliuzwa katika Minada mbalimbali hapa nchini.
Dkt
Mashingo alisema kutokana na mifugo hii jumla ya tani 679,962 za nyama
zimezalishwa ambapo jumla ya tani 1,248.4 za nyama ya mbuzi, tani
1,030.79 za nyama ya ng’ombe, tani 50 za nyama ya kondoo na tani 280 za
nyama punda zenye jumla ya thamani ya dola za kimarekani billioni 5.7
ziliuzwa katika nchi mbalimbali.
Alisema matumizi ya
minada yanawezesha ukusanyaji wa ushuru na tozo mbalimbali kutokana na
biashara ya mifugo hivyo kuchangia katika pato la Taifa na kuiwezesha
Serikali kutekeleza majukumu yake. Uwepo wa minada, hususani ya mipakani
unasaidia katika kudhibiti biashara ya magendo hasa utoroshaji wa
mifugo kwenda nje ya nchi.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Masoko na Huduma za uzalishaji wa Mifugo, Asimwe Lovince alisema
makusanyo ya ushuru na tozo toka minada ya upili na mipakani kwa mwaka
2016/17 yalikuwa 4,775,682,750 ambapo mwaka 2017/18 ni 10,151,124,000
sawa na asilimia 129 ya lengo la makusanyo ya 7,871,000,000/= lililokuwa
limepangwa kukusanywa mwaka 2017/18. Hata hivyo kutokana na uzoefu wa
zoezi la doria ya Operesheni Nzagamba linaloendelea, imedhihirika kuwa
kuna upotevu mkubwa wa makusanyo ya maduhuli ya Serikali.
“Tunafahamu
kuwa Minada yetu imekuwa na changamoto kadhaa zikiwemo za ukosefu na
uchakavu wa miundombinu, wataalamu wachache, ukosefu wa vitendea kazi
ikiwemo vyombo vya usafiri, ukosefu wa fedha za kuendeshea minada na
maeneo ya minada kuvamiwa na wananchi mfano Pugu mnada wenye hekta 1900
hivi sasa zimebaki hekta 108 tu. Wizara ina dhamira ya kuhakikisha kuwa
changamoto hizi zinatatuliwa ili kuhakikisha kuwa minada inafanya kazi
kwa ufanisi. Katika kulitekeleza hilo Wizara imenunua vyombo hivi vya
usafiri ili kuongeza ufanisi wa kazi katika minada. Vyombo hivi pamoja
na mambo mengine vitasaidia kufuatilia watu wanaokwepa ushuru kwa kuuza
mifugo nje ya minada hivyo kuongeza ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali.”
Asisitiza Dkt. Mashingo
Alisema Pikipiki hizi aina ya Honda XL
125 toka Japan zilinunuliwa na Wizara kupitia Wakala wa Serikali wa
Manunuzi (GPSA) kwa thamani ya Sh 83,000,000/= sawa na Sh 8,300,000/=
kila moja.

No comments