Header Ads

Responsive Ads Here

CRDB YAJIPANGA KUKABILINA NA USHINDANI

Viongozi Meza Kuu kwenye Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB uliofanyika leo Mei 19, 2018. Mkutano huo umefanyika Ukumbi wa Simba (AICC) jijini Arusha. (Picha na Yusuph Mussa, Immamatukio Blog).


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei akisoma taarifa yake ya mwaka kwenye Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki hiyo leo Mei 19, 2018. Mkutano huo umefanyika Ukumbi wa Simba (AICC) jijini Arusha. (Picha na Yusuph Mussa, Immamatukio Blog).


Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB uliofanyika leo Mei 19, 2018. Mkutano huo umefanyika Ukumbi wa Simba (AICC) jijini Arusha. (Picha na Yusuph Mussa, Immamatukio Blog).

Na Yusuph Mussa, Immamatukio Blog, Arusha

TAASISI za fedha hasa mabenki yanakabiliwa na ushindani mkubwa kutokana na ongezeko la huduma za kifedha kutolewa na makampuni ya simu.

Suala hilo limechangia kwa kiasi kikubwa kufungwa kwa benki tano, huku nyingine tano zikiwa chini ya uangalizi maalumu.

Ili kukabiliana na ushindani huo, Benki ya CRDB imejipanga kukabiliana na ushindani huo kwa mwaka 2018 ili kuona inapata ufanisi. Na hiyo pia ni kutokana na Serikali kutoa fursa kadhaa kwa mabenki nchini kujiendesha kwa faida.

Hayo yamesemwa leo Mei 19, 2018 na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei wakati anasoma taarifa yake kwenye Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki hiyo uliofanyika Ukumbi wa Simba (AICC) jijini Arusha.

"Kutokana na ushindani mkali kutoka taasisi zisizo za kifedha, hasa huduma za simu za mkononi na changamoto nyingine, benki nyingi ndogo zilikuwa na hali ngumu, na benki takribani tano zilifungwa na Benki Kuu, na benki nyingine tano ziliwekwa chini ya uangalizi maalumu.

"Ili kukabiliana na changamoto za ukwasi na kuongeza kasi ya ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi, Benki Kuu ilipunguza kiwango cha amana ya benki hadi kufikia asilimia nane (8) na kupunguza kiwango cha riba kwa mikopo ya benki za biashara kutoka asilimia 12 hadi tisa" alisema Dkt. Kimei.

Dkt. Kimei alisema kwa maana hiyo benki za biashara zina uwezo wa kukopa fedha hizo serikalini na wao kuweza kuwakopesha wafanya biashara na watu binafsi, hivyo kurudisha mzunguko wa fedha na shughuli za kawaida kwa wananchi.

Hivyo, Benki ya CRDB imejiwekea malengo ya kimkakati kwa mwaka 2018. Mpango mkakati huo wa miaka mitano 2018-2022, una lengo la kuifanya benki ya CRDB na kampuni zake tanzu kuongoza katika kupata faida kwa kukuza ubora wa rasilimali kupitia huduma kwa wateja.

Wateja hao ni wale binafsi, wadogo na wa kati, ikitumia huduma za kidijitali zenye ubora wa hali ya juu, huku wakiahidi kufanya mageuzi makubwa mwaka huu, katika matawi yao kwa lengo la kuongeza ufanisi na tija.

"Lengo kuu mwaka 2018 litakuwa ni kuongeza kasi ya mageuzi ya kidijitali na kupunguza kiwango cha mikopo chefuchefu (isiyo rudishwa kwa wakati) hadi asilimia nane, kuboresha wastani wa kiwango cha gharama na mapato hadi asilimia 58, na kufanya mageuzi ya uendeshaji kwenye matawi ya benki ili kuongeza tija na ufanisi" alisema Dkt. Kimei. 2018-05-18 15:22 GMT+03:00 Imma Mbuguni : HABARI YA LEO MDAU, TAFADHALI POKEA CODES KWA MATUMIZI
PICHANI: Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei akizungumza kwenye semina ya Wanahisa wa benki hiyo. Semina hiyo imefanyika leo Mei 18, 2018 kwenye Ukumbi wa Simba (AICC) jijini Arusha ikiwa ni utangulizi wa Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB kesho Mei 19, 2018. (Picha Zote na Yusuph Mussa, Immamatukio Blog).
Mtoa mada kwenye semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB Dkt. Blandina Kilama iliyofanyika leo Mei 18, 2018 Ukumbi wa AICC jijini Arusha. (Picha na Yusuph Mussa, Immamatukio Blog).Wanahisa wa Benki ya CRDB wakisikiliza watoa mada (hawapo pichani) kwenye semina iliyofanyika leo Mei 18, 2018 kwenye Ukumbi wa Simba (AICC) jijini Arusha, ikiwa ni utangulizi wa Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB kesho Mei 19, 2018. (Picha na Yusuph Mussa, Immamatukio Blog).


Mtoa mada kwenye semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB Grace Joachim. Semina hiyo imefanyika leo Mei 18, 2018 kwenye Ukumbi wa Simba (AICC) jijini Arusha ikiwa ni utangulizi wa Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB kesho Mei 19, 2018. (Picha na Yusuph Mussa, Immamatukio Blog).

Na Yusuph Mussa, Immamatukio Blog. Arusha

WANAHISA wa Benki ya CRDB wameshauriwa kununua hisa kwa wingi ili kuweza kujiletea maendeleo, kwani ununuaji wa hisa hasa wakati kampuni husika imepata mgogoro wa muda mfupi bei yake inashuka.

Hayo yalisemwa leo Mei 18, 2018 na mtoa mada Dkt. Blandina Kilama kwenye Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa (AICC) jijini Arusha.

Dkt. Kilama alisema wanahisa hao wanatakiwa kununua hisa bei zikiwa ndogo na kuuza hisa hizo bei ikiwa kubwa, lakini pia wanatakiwa kununua hisa muda mfupi kabla ya gawio, kwani uhitaji wa hisa hupanda.

"Nunua hisa bei inapokuwa ndogo, uza hisa bei inapokuwa kubwa. Uza hisa kabla ya gawio, kwani uhitaji wa hisa husika hupanda. Na pia nunua hisa muda baada ya dirisha la gawio kufungwa, uhitaji wa hisa husika hushuka. Pia nunua wakati kampuni imepata mgogoro au changamoto ya muda mfupi, kwani bei hushuka, na nunua hisa iwapo thamani inapanda

"Tunawekeza tukiwa na matarajio ya kupata faida katika uwekezaji wetu. Hili laweza kuwa lengo la muda mfupi au mrefu. Changanya hisa za muda mfupi na mrefu, kampuni ambayo inatoa gawio ama ongezeko la thamani, changanya hisa za huduma na viwanda, mfano usafiri na kuchakata vyakula, changanya makampuni mapya na makongwe, kampuni yenye kukua kama ya nishati ama kampuni ambayo imekuwepo muda mrefu" alisema Dkt. Kilama.

Dkt. Kilama amesema watu wengi hawana mpango mkakati wa kimaendeleo, na wenye mkakati huo hawajauandika, hivyo ili mtu kuendelea anahitaji kuweka mkakati ulioandikwa, utamuwezesha kuwa na kumbukumbu, lakini pia kumuwezesha kufanikiwa.

"Tengeneza mpango mkakati binafsi na uutathmini kila wakati. Katika kutekeleza mpango wako wa mwaka, tenga fedha za kutosha kwa ajili ya hisa kila mwezi. Pia katika kutekeleza mpango wako wa kila mwaka, tenga muda wa kutosha kwa ajili ya kutathmini hisa kila mwezi" alisema Dkt. Kilama.

Dkt. Kilama amewataka wanahisa hao kutumia Soko la Hisa kama njia ya kujiongezea mtaji wa awali, kutekeleza maamuzi yako na kuyasimamia na kuona mtu anafanikiwa. Kesho Mei 19, 2018, Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa CRDB ndiyo utafanyika, ambapo mambo mbalimbali ya benki hiyo yatazungumziwa.

No comments