Header Ads

Responsive Ads Here

Wananchi wafunguka Ukarabati Kituo cha Afya Karume Manispaa ya Ilemela


BMG Habari-Pamoja Daima!
Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI ilitoa shilingi milioni 500 na zimetumika kituoni hapo kujenga maabara ya kisasa,chumba cha upasuaji, wodi ya akina mama, chumba cha maiti, nyumba ya mtumishi, choo pamoja na kukarabati majengo ya zamani.
Wananchi katika Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza wamevutiwa na ukarabati wa Kituo cha Afya Karume kilichopo Kata ya Bugogwa na hivyo kuwa na matumaini zaidi ya upatikanaji wa huduma bora za afya kituoni hapo.


Wakizungumza na BMG, baadhi ya wananchi kutoka Kata za Bugogwa na Shibula wanaotegemea zaidi kituo hicho, walieleza kwamba hali ya upatikanaji wa huduma za afya imeboreshwa zaidi baada ya ukarabati huo na kutumia fursa hii kuiomba serikali pamoja na wadau wengine wa afya kusaidia upatikanaji wa vifaa tiba kwenye majengo mapya ikiwemo maabara pamoja na upasuaji.

Mganga Mkuu wa kituo hicho Dkt.Gaspar Lugela alisema ukarabati huo umegharimu takribani shilingi milioni 500 za mfuko wa RBF zilizotolewa na Ofisi ya Rais TAMISEMI na kwamba serikali imeanza kuwasilisha baadhi ya vifaa tiba kituoni hapo.


Kituo hicho kilianzishwa kama Zahanati mwaka 1967 na kilifunguliwa na Rais wa kwanza serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Mzee Abeid Karume na mwaka 2012 kilipandishwa hadhi kuwa Kituo cha Afya hivyo ukarabati huu umekuja muda mwafanya chini ya serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli.

No comments