Header Ads

Responsive Ads Here

Vituo binafsi vya Afya Mwanza vyasaini makubaliano ya kutoa bure huduma kwa wananchi

BMG Habari-Pamoja Daima!
Watoa huduma za afya binafsi Jijini Mwanza leo Machi 20,2018 wamesaini Mkataba wa Mashirikiano baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ili kutoa bure huduma za afya kwa upande wa akina mama na watoto.
Mpango huu unaratibiwa na Chama cha Watoa Huduma za Afya Binafsi Tanzania APHFTA kupitia ufadhili wa shirika la Pharmaccess International.
Makubaliano haya yatasaidia uboreshaji wa huduma za afya kwa upande waa mama na mtoto katika vituo binafsi vya afya.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe.Marry Tesha akizungumza kwenye hafla hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella.
Mganga Mkuu mkoani Mwanza, Dkt.Leonard Subi akizungumza kwenye hafla ya kusaini makubaliano hayo.
Mratibu wa Ushirikiano baina ya sekta binafsi na ya umma idara ya Afya kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Jumanne Mwasamila akiwasilisha salamu kwenye hafla hiyo.
Mratibu wa Ushirikiano baina ya sekta binafsi na ya umma idara ya Afya kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Mariam Ongana akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Watoa Huduma za Afya Binafsi Tanzania APHFTA Dr.Samwel Ogillo akizungumza kwenye hafla ya kusaini makubaliano hayo.
Mratibu wa APHFTA Kanda ya Ziwa, Dr.Joyce Mwihava akijitambulisha.No comments