Header Ads

Responsive Ads Here

SUMATRA kuanzia safari mpya za mabasi madogo Jijini Mwanza


Judith Ferdinand,  BMG
Abiria wanaotegemea usafiri wa barabara katika eneo la Usagara wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, wanatarajia kupata neema ya usafiri wa moja kwa moja katikati ya Jiji la Mwanza.
Hayo yalisemwa jana na Afisa Leseni na Mkaguzi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) mkoa wa Mwanza, Daniel Chilongani  kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) Mwanza.
Kikao hicho kilichohudhuriwana viongozi mbalimbali wa serikali, dini na wanasiasa kilichofanyika mkoani hapa  alisema wapo katika hatua za awali za kuanzisha safari za daladala ambazo zitakuwa za Usagara – Mzunguko zitakazokuwa zinapita katikati ya jiji na kuishia hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure.
Chilongani alisema wameamua kuja na mpango wa  kuanzisha safari (roote) hiyo ili kuwasaidia   na kutatua changamoto ya usafiri kwa  wananchi wa Usagara, kwani wakitaka kupata huduma katika hospitali ya mkoa   wanatumia gharama kubwa kwa ajili ya nauli  na wanapata usumbufu wa kutumia gari zaidi ya moja kufika eneo husika.
Alisema Sumatra katika kuhakikisha inaondoa hadha ya usafiri kwa wananchi wanategemea kuanzisha safari (roote) nyingine ambayo itatoka Kigongo Ferry kupitia  katikati ya jiji hadi hospitali ya  mkoa ambapo magari yatakuwa ni Kigongo Ferry – Mzunguko ambayo yatahusisha  magari makubwa ( mabasi makubwa) yenye uwezo wa kubeba abiria kuanzia 25.
Pia alisema safari (roote) hiyo itasaidia kupunguza msongamano wa daladala katikati ya mji pamoja na kuwapa fursa wananchi ya kupata usafiri  na kusafirisha bidhaa zao kwa urahisi, ili waweze kuendelea katika shughuli za kimaendeleo na kupata huduma muhimu zinazipatikana makao makuu ya mkoa.
Naye Mwenyekiti wa  Chama Cha Madereva Kanda ya ziwa, Hassan Dede alisema sumatra wanapoanzisha  safari (roote) mpya washirikiane kwa pamoja  katika kuhakikisha wanaelimisha madereva  na kubandika  stika zinazoonyesha  mwanzo hadi mwisho wa safari.

No comments