Header Ads

Responsive Ads Here

RC Mwanza Mwanza ataka wananchi waelimishwe kuhusu Bima ya Afya


Judith Ferdinand, BMG
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amewataka Wenyeviti wa Halmashauri na viongozi mbalimbali wa mkoa kuweka utaratibu wa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhumi wa bima ya afya.
Aliyasema hayo jana kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) kilichohudhuliwa a viongozi mbalimbali wa Serikali ,dini na wanasiasa, alisema ni vema kuhakikisha wananchi wanapatiwa elimu ili waweze kutambua umuhimu wa  kutumia bima ya afya.
Mongella alisema anasikitika kuona watu hawatambui muhimu wa kujiunga na bima ya afya kwani  hurahisisha matibabu na gharama yake ni ndogo tofauti na mtu ambaye hatumii huduma hiyo.
Alisema ili kuweza kupunguza vifo kwa wananchi ni vema kila kiongozi kuweka utaratibu wa kuelimisha jamii katika maeneo yao lengo ikiwa kupunguza na kumaliza tatizo hilo kwani watapata matibabu wakati wote.
“Ili tuweze kupunguza vifo vya watoto na wananchi kwa ujumla ni vema kuweka utaratibu wa kuwaelimisha wananchi kuhusu kutumia bima ya afya kwani inasaidai pindi ukiwa hauna hela na unaumwa au kuuguliwa,”alisema Mongella.
Pia alisema, ni dhambi kutoa hamasisha wananchi kuhusu  kutambua faida ya bima ya afya ambayo ni mkombozi  kwa wenye hali ya chini kwani hutumia pesa nyingi katika matibabu wakati viongozi wanatumia na wamejiunga  huduma hiyo.
Naye Clement Pancras Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Part (DP) alisema ni vema kwa viongozi kuhamasisha wananchi katika mambo ya msingi ikiwemo bima ya afya kwa ustawi wa maisha yao na taifa kwa ujumla.
Alisema  kila mwanachi atakapokuwa na bima itasaidia hasa wenye hali ya chini ingawa changamoto iliyopo ni hupatikanaji wa dawa ambao itamlazimu mgonjwa kutoa fedha za kununulia, hivyo aliiomba serikali kupeleka na  kuhakikisha  dawa zote zinapatikana  katika hospitali  zote na kuleta maana halisi ya kutumia huduma hiyo.

No comments