Header Ads

Responsive Ads Here

Mradi wa VUGUVUGU LA TAI kwa Wasichana wazinduliwa Jijini Mwanza


BMG Habari-Pamoja Daima!
Shirika la Mikono Yetu limezindua rasmi mradi wa Vuguvugu la Tai (Eagle Movement For Adolescent Girls) kwa wasichana wa Jiji la Mwanza, unaolenga kuwawezesha na kuwajengea uwezo wasichana katika shule za sekondari ili kujitambua na kutimiza malengo yao.
Mradi huo wenye kauli mbiu isemayo “Mwanamke ni Tai sio Kuku” umezinduliwa hii leo katika shule ya sekondari Buswelu, ambapo utekelezaji wake wa majaribio unahusisha wanafunzi wa kike kutoka shule hiyo pamoja na shule ya sekondari Bujingwa zilizopo Ilemela Jijini Mwanza
Mradi huo ulitambulishwa mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana na utafikia tamati mwezi Septemba mwaka huu chini ya ufadhili wa taasisi ya “Novo Foundation”, ambapo hadithi za wanawake mbalimbali waliofanikiwa tangu karne ya 16 zitatumika kuwahamasisha wasichana ili kutambua wao ni thabiti na shujaa kama ilivyo kwa ndege Tai hivyo wakunjue mbawa zao na kuruka kuelekea kwenye mafanikio badala ya kutulia kama kuku.


No comments