Header Ads

Responsive Ads Here

Mkurugenzi wa Africa Insight Advisors awatembelea Wawekezaji Mwanza

BMG Habari-Pamoja Daima!
Mkurugenzi wa taasisi ya Africa Insight Advisors ya nchini Marekani ambayo pia ina ofisi zake Jijini Dar es salaam, Alexander Howe leo amefanya ziara ya kuwatembelea wawekezaji mbalimbali mkoani Mwanza na kujionea fursa za uwekezaji.
Mkurugenzi huyo ameambatana na mwenyeji wake, Patrick Tungu ambaye ni Mkurugenzi wa taasisi ya TAWESO ya Jijini Mwanza, ambapo pia amekutana na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi Eliurd Mwaiteleko na kuzungumzia fursa mbalimbali za uwekezaji wilayani humo.
Mkurugenzi wa taasisi ya Africa Insight Advisors, Alexander Howe pamoja na wenyeji wake wamemtembelea Mkurugenzi wa kampuni ya Kipipa Millers Ltd.
Patrick Tungu ambaye ni Mkurugenzi wa taasisi ya TAWESO, akiagana na Mkurugenzi wa kampuni ya Kipipa Millers Ltd ya Jijini Mwanza, Oliver Matemu (kulia).
Ugeni huu pia umefika wilayani Magu na kukutana na Matiko James (kulia) ambaye anatarajia kuanzisha kiwanda cha ngozi na mafuta ya kula wilayani humo.
Ugeni huu umekutana na Mkurugenzi wa kampuni ya Double D inayozalisha Ice Cream Jijini Mwanza (kulia).
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi, Eliurd Mwaiteleke akizungumza na Mkurugenzi wa taasisi ya Africa Insight Advisors, Alexander Howe pamoja na Patrick Tungu ambaye ni Mkurugenzi wa taasisi ya TAWESO.
Mazungumzo yakiendelea.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi, Eliurd Mwaiteleke akifafanua jambo wakati wa mazungumzo hayo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi, Eliurd Mwaiteleke akizungumza na Alexander Howe.Bonyeza HAPA kwa habari zaodi.

No comments