Header Ads

Responsive Ads Here

Kongamano la Maombi Maalumu ya kuombea Taifa

Na BMG Kituo cha Maombi, Ushauri na Neno la Mungu kinawakaribisha watu wote kwenye Kongamano la Maombi Maalumu ya kuombea Mkoa wa Mwanza na Taifa kwa ujumla. Kongamano hili litafanyika siku ya jumapili Machi 11,2018 kuanzia majira ya saa 15:00 mchana hadi saa 18:00 jioni, mahali ni Pasiansi Mtaa wa Iloganzara barabara inayoelekea kiwanda cha Breweries kilipo kituo cha Maombi, Ushauri na Neno la Mungu. Waimbaji mbalimbali wakiwemo Moses Butoi (Mzee wa Drip), Emmanuel Mwasasumbe, Andrew Samson, Derick Ndonge, Julieth Bisangi pamoja na kwaya kama vile Gilgal Choir, FPCT Pasiansi, AIC Pasiansi na nyingine nyingi zitatumbuiza kwenye kongamano hili. Kumbuka kongamano hili halina kiingilio, yaani ni bure kabisa hivyo njoo ili kwa pamoja tuombee Baraka, Amani na Mafanikio ya mkoa wetu wa Mwanza na Taifa kwa ujumla. Kwa msaada zaidi, wasiliana nasi kwa nambari za simu 0767 77 76 17. WATU WOTE, KWA IMANI ZOTE, NJOONI TUMWOMBE MUNGU KWA AJILI YA TAIFA LETU TANZANIA.

No comments