Header Ads

Responsive Ads Here

CRDB YAISAIDIA SERIKALI YA DKT MAGUFULI KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA , YAWAFIKIA MAWAKALA WA FAHARI HUDUMA 300

Mkurugenzi  wa  CRDB  mkoa  wa  Iringa  Kissa  Samweli  akizungumza na  wanahabari
Mwezeshaji  Sophia  Nyoni  akitoa  semina  kwa  mawakala  wa  fahari  Huduma

 Wakala  maarufu  wa  fahari  huduma  Iringa  Frank  Mdesa  akieleza  faida ya  huduma  hiyo
......................................................................................................................
Na  MatukiodaimaBlog

MAWAKALA wa  fahari  huduma  kupitia  benki ya  CRDB mkoani  Iringa wamepongeza benki   hiyo  kwa kuanzisha   huduma  hiyo  ambayo  imesaidia  kukuza  ajira  kwao  na  kwenda  sanjari na mkakati wa  Rais  wa awamu ya  tano  Dkt  John Magufuli   wa  uwezeshaji .
Wakizungumza  mara  baada ya  mafunzo ya  siku  moja  ya  kuwaongezea  ujuzi  zaidi  watoa  huduma  wa  fahari  huduma  Tulipo  tupo  washiriki  wa  warsha  hiyo  walisema  kuwa   kuanzishwa  kwa  huduma   hiyo  si  tu  kumepunguza wateja  kusafiri   mwendo  mrefu  kufuata  huduma   hiyo  ila  kumeongeza   ajira  zaidi  kwa  vijana  na  wengi  wao  kuwa ni sehemu ya  watenda kazi wa  CRDB .
Mtoa  huduma  kutoka  Kalenga  Felista  Juma  alisema  kuwa  huduma   hiyo  ya  fahari    huduma    imesaidia  kuwezesha  wananchi  kulipa  ada  kwa  haraka  zaidi  pamoja na kufanya  mihamala ya  kifedha  na  kwake  imemuongezea  kipato  zaidi  kwa mihamala  aliyoifanya .
Felista  alisema  kuwa  kwa  upande  wake  amesomea  uhasibu  ila  hakuwa na ajira    hivyo  kwa  kupitia  uanzishwaji  huo  wa fahari  huduma  ameweza  kupata  ajira  na  hivyo  kinachofanywa na  CRDB ni  kuisaidia  serikali  kuongeza  ajira  .
  CRDB  imeleta  ajira  kwa  wasio na ajira  imeisaidia  serikali  kuelekea  serikali ya  viwanda  maana  kazi  hii ya  huduma  za  kifedha  ni  zaidi ya  viwanda”
Julieti  Mkalimoto   kutoka  mjini  Iringa alisema  kuwa huduma ya  fahari  huduma  ni  huduma  nzuri  ambayo  kwa  Tanzania ya  viwanda  mtu  kukaa bila  kazi  ni shida  hivyo  alisema  kwake  ameweza  kutunza  familia yake kwa  kupitia  huduma  hiyo  pamoja na  kujulikana  zaidi kwa  wateja .
Wile Kamwela  ni  kutoka  CRDB  makao makuu  kitengo  cha elimu ya masoko  kwa  wateja  alisema  kuwa moja kati ya  mada  kuu katika warsha  hiyo  ilikuwa ni  kuwajengea  uwezo na  uboreshaji  wa  huduma  kwa mawakala  hao kwa  lugha  yenye  mvuto  zaidi .
Kuwa lengo  ni kutaka  wateja  kuvutiwa na  huduma  hiyo na  kutoonyesha  tofauti kati ya  tawini na  kwa  mawakala  hao .
Alisema kuwa mawakala  hao  ni  watumishi wa CRDB  hivyo  wasingependa  kuona  wanakiuka  kanuni  za utoaji wa  huduma  bora na  wao  hawawi  sehemu ya  kuichafua  benki kwa  kutoa  huduma  iliyochini ya  kiwango.
Kamwela alisema hadi  sasa CRDB inajumla ya  mawakala wa  fahari  huduma  zaidi ya  3000 nchi  nzima na  kuwa lengo la  benki  hiyo ni  kuendelea  kuongeza  idadi ya mawakala  zaidi  ili  wateja  wasipate  shida .
Mkufunzi  Sophia  Nyoni kutoka CRDB  Iringa alisema ndani ya  mkoa  wa Iringa  kuna zaidi ya mawakala  70  ambao  wamesajiliwa  kufanya kazi  hiyo .

Kuwa  wito  kwa  wafanyabiashara  kujiunga na  uwakala  wa fahari  huduma  na  kuwa ili  kuwa  wakala  lazima  uwe  umekaa eneo  husika  kwa  zaidi ya  miaka  miwili  eneo  moja na kuwa na barua  toka kwa  viongozi wa serikali za  mitaa na  kuwa uwakala unatolewa kwa  kila mtu hata  taasisi  za  serikali .
Kisa  Samweli ni Mkurugenzi wa CRDB mkoa  wa  Iringa  alisema  kuwa  benki   hiyo  inaungana na  serikali na  harakati  zake  kuona  wananchi  wengi  wanafikiwa na  huduma  za  kifedha pamoja na  kuona benki  hiyo  inamuunga mkono  Rais Dkt  Magufuli  kuelekea  Tanzania ya  viwanda ambayo kutekelezwa kwake  inahitaji  huduma  za  kifedha  kuwafikia  zaidi .
Alisema  kuwa  toka  huduma  hiyo  imeanza kasi ya  wateja  kujiunga na  CRDB  imekuwa  kubwa zaidi  na  kuwa  CRDB ni moja kati ya  benki  bora  nchini  na  wito  wake  ni wateja  kuendelea  kujenga  imani kwa  mawakala  hao  kwani  wanachujwa na  wanaaminiwa  na  benki  kuu ya Tanzania (BOT).No comments