Header Ads

Responsive Ads Here

SHEREHE ZA POLICE FAMILY DAY 2018 SHINYANGAJeshi la polisi mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Februari 5,2018 limefanya sherehe ya Siku ya Polisi na Familia ‘Police Family Day’ kuuaga na mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka 2018.

Sherehe hizo zimefanyika katika viwanja vya polisi Kambarage Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.

Sherehe hizo zimehudhuriwa na maafisa wa polisi,wakaguzi,askari wa vyeo mbalimbali na wadau wa usalama wananchi mkoa wa Shinyanga. 

Mgeni rasmi Josephine Matiro amekagua gwaride maalum,maonesho mbalimbali kukabidhi hati za sifa na pongezi kwa askari waliofanya kazi vyema mwaka 2017 katika ulinzi na usalama wa mkoa wa Shinyanga lakini pia hati zimetolewa kwa wadau mbalimbali walioshirikiana na jeshi la polisi katika kuimarisha usalama mkoani humo. 

Mgeni rasmi pia amefungua kituo cha polisi kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Shinyanga kilichopo katika kituo cha polisi wilaya hiyo. 

Mwandishi Mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametusogezea picha 76 za matukio yaliyojiri…tazama hapa chini
Askari polisi mkoa wa Shinyanga wakiwa katika viwanja vya Polisi Kambarage mjini Shinyanga wakati wa sherehe za "Police Family Day" leo Jumatatu Februari 5,2018 - Picha zote na Kadama Malunde 
Askari polisi wa kikosi cha usalama barabarani wakiwa katika viwanja vya polisi Kambarage Mjini Shinyanga 
Mgeni rasmi, mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akipokelewa na Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule katika viwanja vya polisi Kambarage mjini Shinyanga. 
Mgeni rasmi akijiandaa kukagua gwaride maalumu lililokuwa linaongozwa Mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) Abwao Richard 
Vikosi vikiwa katika gwaride.. 
Kushoto ni Mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) Abwao Richard akitoa ripoti kwa mgeni rasmi 
Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akikagua gwaride 
Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akikagua gwaride 
Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akikagua gwaride
Askari wakiwa wamebeba silaha 
Askari waliokabidhiwa hati za sifa na pongezi kwa kulitumikia vyema jeshi la polisi mwaka 2018 wakielekea kwa mgeni rasmi kupokea hati 
Mgeni rasmi Josephine Matiro akikabidhi hati ya sifa na pongezi kwa mmoja wa maaskari polisi waliotekeleza vyema zaidi majukumu yao mwaka 2017 
Zoezi la kukabidhi hati kwa askari polisi waliotumikia vyema zaidi jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga likiendelea 
Kennedy Abdul akipokea hati ya sifa na pongezi 
WP Safina akipokea hati ya sifa na pongezi 

Kiongozi wa gwaride akitoa maelekezo ya kabla ya askari kupita mbele ya mgeni rasmi kutoa heshima 
Kikosi cha FFU kikitoa heshima kwa mgeni rasmi 
Mgeni rasmi na meza kuu wakiwa wamesimama wakati vikosi vikitoa heshima kwa mgeni rasmi Josephine Matiro 
Wageni waalikwa wakiwa eneo la tukio 
Askari wa JWTZ wakiwa katika sherehe hizo 
Viongozi wa CCM na wananchi wakiwa katika sherehe hizo
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akizungumza wakati wa sherehe za Police Family Day 
Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akikabidhi hati ya sifa na pongezi kwa mmoja wa wadau walioshiriki kuimarisha ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga 
Sheikh wa mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akipokea hati ya sifa na pongezi 
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Msalala Simon Berege akipokea hati ya sifa na pongezi 
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde akipokea hati ya sifa na pongezi 
Zoezi la kugawa hati za sifa na pongezi likiendelea 
Mwakilishi wa Kom Sekondari Jackton Koyi akiwa ameshikilia hati ya sifa na pongezi 
Mwakilishi wa shule ya Little Tresures Mwita akipokea hati ya sifa na pongezi 
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Said Pamui akipokea hati ya sifa na pongezi 
Mwenyekiti wa mtaa wa Miti Mirefu mjini Shinyanga Nassoro Warioba akipokea hati ya sifa na pongezi
Mwakilishi wa mwanasheria mkuu wa serikali akishikana mkono na katibu tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela 
Kwaya ya AICT Kambarage ikitoa burudani 
Mbunge wa jimbo la Kishapu Suleiman Nchambi akipokea hati ya sifa na pongezi 
Sherehe zinaendelea 
Wadau wakiwa eneo la sherehe 
Sherehe zinaendelea 
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akizungumza wakati wa sherehe hizo 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza katika sherehe hizo 
Kikosi cha mbwa na farasi wakionesha namna ya kukamata mhalifu kwa kutumia mbwa 
Kikosi cha judo na kung fu kikionesha namna wanavyopambana na wahalifu 
Sherehe zinaendelea 
Dawati la jinsia na watoto wakionesha igizo kuhusu mimba na ndoa za utotoni 
Askari polisi wakionesha namna ya kupambana na majambazi 
Askari polisi wa usalama barabarani wakionesha namna wanavyoshughulika na wavunjifu wa sheria za barabarani 
Wadau wakiwa eneo la tukio 
Vijana wa sarakasi wakionesha kipaji chao 
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba akizungumza katika sherehe hizo 
Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akitoa hotuba wakati wa sherehe za police family day 
Josephine Matiro alisema serikali inalipongeza jeshi la polisi kwa kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama katika mkoa wa Shinyanga 
Mgeni rasmi akitoa hotuba yake 
Wadau wakiwa katika eneo la tukio 
Waandishi wa habari wakiwa katika sherehe hizo 
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mkoa wa Shinyanga na maafisa wa kikosi cha usalama barabarani 
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mkoa wa Shinyanga na wadau mbalimbali 
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mkoa wa Shinyanga na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama 
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mkoa wa Shinyanga na viongozi wa CCM 
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mkoa wa Shinyanga na wajumbe wa kamati ya maandalizi ya sherehe hizo 
Picha ya kumbukumbu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Simon Haule na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama 
Picha ya kumbukumbu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Simon Haule na maaskari wa JWTZ 
Picha ya kumbukumbu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Simon Haule na maaskari magereza 
Picha ya kumbukumbu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Simon Haule na maaskari wa kikosi cha zimamoto na uokoaji 
Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiwa katika banda la polisi kitengo cha TEHAMA akiangalia vifaa wanavyotumia katika mawasiliano 
Afisa TEHAMA jeshi la polisi akitoa maelezo kwa mgeni rasmi 
Jengo la ofisi ya kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Shinyanga
Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizindua jengo la ofisi ya kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Shinyanga 
Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akikata utepe wakati akizindua jengo la ofisi ya kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Shinyanga 
Mgeni rasmi Josephine Matiro akiwa ndani ya jengo la ofisi ya kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Shinyanga 
Picha ya pamoja nje ya jengo la ofisi ya kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Shinyanga 
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Simon Haule akizungumza nje ya jengo la ofisi ya upelelezi wilaya ya Shinyanga linaloendelea kujengwa.

No comments