Header Ads

Responsive Ads Here

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA DR SLAA NA MBOWETO KUWA MABALOZI WA SWEDEN, NIGERIALeo Februari 16, 2018 Rais John Magufuli amewaapisha mabalozi wawili aliowateua kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Nigeria na Sweden.

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi inaeleza kuwa walioapishwa ni Muhidin Ally Mboweto ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria na Dk Willbrod Peter Slaa ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden.

Uteuzi wa Mabalozi hao kuiwakilisha Tanzania katika nchi walizopangiwa umeanza jana Februaru 15, 2018.

No comments