Header Ads

Responsive Ads Here

MGODI WA GGM WAPEWA SIKU 2 KUANZA MCHAKATO KUWAFIDIA WANANCHI

Naibu  waziri  wa madini Stanlaus Nyongo Akizungumza na  Wakazi  Wa Kijiji Cha Nyakabale  wakati wa ziara yake Mkoani Geita.


Naibu  waziri  wa madini Stanlaus Nyongo akishiriki zoezi la kupanda mawe ya dhahabu.

Naibu  waziri  wa madini Stanlaus Nyongo akizungumza na diwani wa kata ya Mgusu Patory Ruhusa.

Naibu Waziri  Akimsikiliza Pili Mwaluko Anaefanya Kazi Ya Uchenjuaji Madini kwenye mtaa wa Nyakabale. 

Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa pamoja na Naibu Waziri  wa madini Stanlaus Nyongo.


Na,Joel Maduka,Geita.


Naibu  waziri wa madini  Stanslaus Nyongo amesema kuwa serikali ya awamu ya tano haiko tayari  kuona mtu akilalamika ,kunyanyaswa au kunyimwa haki yake.

kauli hiyo ameitoa wakati akiongea na wananchi wa kijiji cha Nyakabale  kata ya  Mgusu  Wilayani Geita wakati wa ziara yake ya siku mbili Mkoani humo ya kuzungukia maeneo ya uchimbaji pamoja na kusikiliza kero za wananchi ambao wanazunguka kwenye baadhi ya maeneo ya mgodi wa Geita(GGM).

Hatua  hiyo ya Naibu waziri Nyongo imekuja baada ya kusikia malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya mgodi wa GGM kushindwa kuwalipa fidia kwa muda mrefu pamoja na kuwepo kwa maagizo mengi ambayo yamekuwa yakitolewa na baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakifika Mkoani Humo.

Naibu waziri huyo alisema kuwa mtu mwingine yuko tayari kuona Mtanzania mwenzake akikandamizwa ilimradi yeye  aendelee kulinda masilahi yake  binafsi, na kwamba miaka hiyo imeshapita muda uliopo kwa sasa ni kufanya kazi za kuwatumikia wananchi ambao ni wanyonge.

 “Tukikaa kwenye viyoyozi hatuambiwi ukweli na wamiliki wa migodi lakini tunapo fika katika eneo husika tunapata ukweli , unakuta mtu kazaliwa hapo kakulia hapo amejenga ana watoto harafu mtu anakuondoa kwa madai kuwa upo kwenye leseni yake  ainiingi akilini kama unahitaji eneo langu njoo tukae tumalizane  unipe changu mimi nisepe inakuwa nilipe nisepe ”alisema Nyongo.

Hata hivyo aliwataka watu wa mgodi huo kuwalipa wananchi hao ama waondoke wawaachie wananchi hao eneo lao waendelee kuchimba na sio kuwazuia ikiwa hawafanyi shughuli za uchimbaji kwa sasa au wawaache waendelee kufanya shughuli za bila kubuguziwa,  mgodi ulikuja kama neema hivyo isiwe mgodi huu kazi yake  kuwanyanyasa wananchi.

Awali Akitoa malalamiko kwa Naibu waziri  mwananchi wa Nyakabale kwa niaba ya wenzake Joseph Kihengu alimwambia Naibu waziri  kuwa wanailaumu serikali iliyopita  inawezekana wakati wanabinafsisha mgodi huu na wao waribinafisishwa humo bila kujua.

“Mheshimiwa   kipindi cha nyuma usingeweza kupata umati kama huu, umati huu umetokana na imani ya serikali ya awamu ya tano waliyo nayo hivyo serikali iwaangalie kwa jicho la tatu ili watu wanyakabele  wajue hatima ya maeneo ambayo yapo ndani ya bikoni mgodi wa GGM”Alisema Joseph.

Katika hatua nyingine akina mama wa nyakabale wakiwakilishwa na Godliva Mgini waliutupia lawama mgodi huo wa GGM kwa kuwafilisi kwa kukilaghai kikundi chao cha Baraka baada ya  kuwaahidi kuwawezesha kuanzisha  mradi ufungaji  wa nguruwe 100 ambapo waliambiwa wasombe mawe ili wajenge na kujikuta wakighalamia  kiasi cha shilingi laki nane  baadae wakatokomea kusiko julikana na kuwaacha maskini zaidi.

Nae  makamu wa rais GGM Saimon Shayo alisema “tunatambua majirani hivyo niseme tu baadhi ya maneno yaliyoelezwa hapa mengine yanafahamika mengine ni mageni ndo tunayasikia na mangine tunahitaji   kama mgodi kukaa na kuyapatia ufumbuzi”.

Aidha alisema kuwa kuna baadhi ya watu wa nyakabale vigingi vyao vipo ndani ya mgodi ambapo  kimsingi  jambo ili lipo wazi pia kuna watu wana haki ya ardhi kisheria suala  na kwamba suala hilo  ni namna  ya kukaa pamoja  na kujadili kwasasa.

No comments