Header Ads

Responsive Ads Here

MCHANGO WA MAKTABA KUELEKEA KWENYE SERIKALI YA VIWANDA

Na: Calvin Edward Gwabara
Songea - Ruvuma.


CHAMA cha wakutubi Tanzania (TLA) kimeiomba Serikali na wadau wa elimu nchi kusaidia kupatikana kwa Maktaba kwenye shule zote za msingi na Sekondari nchini ili kuweza kuwajengea watoto tabia ya kujisomea angali wakiwa wadogo kupitia maktaba hizo.
 
Mwenyekiti wa TLA Dkt. Juliana Manyerere akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mkutano huo.
Ombi hilo limetolewa Mwenyekiti wa chama hicho kwa niaba ya wakutubi wote nchini Dr. Juliana Manyerere wakati akitoa hutuba yake kabla ya kumkaribisha mkuu wa wilaya ya Songea Mhe. Poloreti Komando Mgema kufungua mkutano wa mwaka wa wananchama wa chama hicho kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo  unaofanyika mkoani Ruvuma.

Alisema maktaba zina manufaa makubwa katika kusaidia watu kupata maarifa hivyo zina umuhimu mkubwa kuwepo kwenye kila shule tofauti na hivi sasa ambapo shule nyingi hazina maktaba hali ambayo inawafanya wanafunzi kukosa ari na kujijengea mazoea ya kujisomea wakiwa katika ngazi za chini.


Dr. Manyerere alisema kuwa (TLA) imefanya kazi kubwa tangu kuanzishwa kwake ikiwemo kuwakutanisha wakutubi kupitia chama hucho na kujadiliana mambo mbalimbali yenye lengo la kuboresha taaluma hiyo lakini pia kutoa huduma za ushauri kwenye shule,vyuo na taasisi juuu ya namna nzuri ya kutuzna vitabu na machapisho pamoja na kutoa huduma bora kwa wasomaji wa vitabu.
Wakutubi kutoka nchi nzima wakifuatilia hutuba za ufunguzi wa mkutano wao.


‘’ Tunaiomba pia Serikali kuona umuhimu wa kuajiri wakutubi wenye taaluma kwenye shule zetu nchini na kwenye maofisi ya serikali ili waweze kutoa huduma kitaalamu tofauti na hivi sasa ambapo maktaba nyingi zimeonekana kuwa wakutubi ambao sio wanataaluma hiyo ingawa wanatoa huduma kwa wahitaji’’ Alisisitiza Dr. Manyerere.

Dr. Manyerere alisema wanaamini kuwa katika kuelekea Tanzania ya Viwanda fani ya ukutubi na Maktaba ina mchango mkubwa katika kusaidia serikali kutekeleza mpango huo wa serikali ya awamu ya tano kwakuwa maarifa na taarifa nyingi kuhusu mpango huo zinapatikana kwenye maktaba zetu nchini.

Mwenyekiti huyo wa chama cha wakutubi Tanzania  pia alisema pamoja na kuwa na uwezo mdogo wa fedha za kutekeleza mikakati mbalimbali ya chama hicho kwa manufaa ya taifa lakini hivi karibuni wametoa mafunzo kwa wakutubi wote kwenye shule za mkoa wa Dodoma na wataendelea kufanya hivyo kwenye mikoa mingine kadri viongozi wa mikoa na wilaya watakavyoshirkiana na chama chao katika kujengea uwezo watumishia wao.

Hata hivyo alisema katika mkutano huu mkuu na mafunzo wamepanga kutembelea shule za sekondari za Songea Boys na Songea Girls kuona namna wanavyotumia maktaba zao na kuwashauri lakini pia kuwapatia zawadi ya vitabu kwaajili ya masomo mbalimbali kama sehemu ya mchango wao lakini pia vitabu 20 vya sayansi  kwa chuo cha VETA Songea  baada ya maombi ya mkuu wa chuo hicho kwenye mkuatano huo.

Akifungua Mkutano mafunzo hayo yanayokwenda sambamba na mkutano mkuu wa chama hicho mkuu wa wilaya ya Songea  Mhe. Poloreti Mgema  kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma  amepongeza kazi kubwa  na mafanikio yaliyopatikana kwenye chama hicho katika kusaidia kuongeza ari ya watanzania kujisomea .
Mkuu wa wilaya ya Songea Mhe. Poloreti Mgema akifungua mkutano huo wa wakutubi unaofanyika Mkoani Ruvuma.


Alisema Maktaba kama chanzo kisima cha maarifa ni muhimu kikatambuliwa na wananchi wengi zaidia na kuhamasishwa kuzitumia kupata taarifa muhimu na sahihi ambazo zimefanyiwa utafiti kwaajili ya kujibu maswali mbalimbali yanayowakabili katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo,Madini,Sayansi na zinginezo.

’’ Niwahakikishie kuwa Serikali inaendelea na jitihada za kuongeza maktaba kwenye shule za msingi na Sekondari  kadri fedha zinapopatikana ingawa  huenda shule za msingi zikachelewa kupata maktaba zote lakini shule za sekondari zitafikiwa haraka na kupatiwa maktaba zenye vitabu stahiki kwa masomo na mahitaji ya wanafunzi hao’’ Alisema Mhe. Poloreti Mgema.

Katika hatua nyingine kijibu changamoto ya fedha inayokikabili chama hicho katika kutimiza majukumu yake aliwashauri kuandika maandiko mbalimbali kwa wadau wa ndani na nje ya nchi ambao wanamapenzi mema na wenye kuona umuhimu wa makataba na kujisomea ili kupata fedha za kusaidia kuwezesha kuendesha kazi za chama kwa ufanisi.
Wakutubi wakifuatilia hutuba za ufunguzi

Mkuu huyo wa wilaya ya Songea Mhe . Mgema amewaomba waajiri wa wakutubi hao na wengine nchini kuwapa nafasi na kuwawezesha wataalamu hao kwenye taasisi na ofisi zao kuhudhuria mikutano na mafunzo ya aina hiyo ambayo yanwapa nafasi wakutubi hao kukutana kwa pamoja na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo mafanikio na changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ili kutoa huduma kwa ufanisi.

Katika mkutano huo Mkurugenzi wa Maktaba ya taifa ya Kilimo kutoka chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof Alfred Sife alitoa mada kuhusu sheria ya upataji wa habari yaani ‘’ The access to information Act,2016’’ na Changamoto zake katika ukutubi Tanzania huku Dkt. Philbert Nyinondi pia toka SUA akiwasilisha mada ya mchango wa Maktaba katika kuelekea Serikali ya Viwanda ‘’The role of Library and information Services in Promoting indunstrilization in Tanzania’’.

Mkutano wa mwaka huu una kauli mbiu na una lenga kujadili ’’ Mchango wa Maktaba na taarifa katika kusaidia kuelekea Tanzania ya viwanda’’.
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo

Daudi Danda mratibu katika mkutano huo akitoa neno kwa washiriki.

Mzee Fabian Kadamah mkutubi mkongwe akitoa neo la shukrani kwa  mgeni rasmi.

Mkurugenzi wa Maktaba ya taifa ya Kilimo kutoka chuo kikuu cha sokoine cha kilimo SUA  Prof. Alfred Sife akiwasilisha mada yake

Washirki wa mkutano huo wakifuatilia mafunzo

Mkuu wa wilaya ya Songea Mhe. Poloreti Mgema (Wa kwanza kulia) na Mwenyekitiwa chama cha wakutubi tanzania TLA Dkt. Juliana Manyerere wakifuatilia utambulisho wa washiriki.

Viongozi wakiwa meza kuu na mkuu wa wilaya wakati wa ufunguzi wa mkutano huo

Dkt. Grace Msoffe (wa kwanza kulia) na Dkt. Pgilbert Nyinondi (wa pili kutoka kulia) wakifuatilia mkutano huo.


Washiriki wa mkutano wakifuatilia mada zinazowasilishwa na wataalamu wa masuala ya ukutubi.

No comments