Header Ads

Responsive Ads Here

KATIBU MKUU DKT. MARIA SASABO AFUNGA MKUTANO WA BARAZA KUU LA WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA (TPC) JIJINI DAR ES SALAAM

Katibu Mkuu (Mawasiliano), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Maria Sasabo (kushoto), akifurahia jambo pamoja na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang’ombe (wa pili kushoto), Kaimu Meneja Mkuu Rasilimali za shirika, Macrice Mbodo (wa tatu) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Elia Madulesi, wakati alipowasili Makumbusho ya Taifa kwa ajili ya kuufunga mkutano wa Baraza Kuu la wafanyakazi wa TPC, jijini Dar es Salaam jana.
Kaimu Postamasta Mkuu wa TPC, Hassan Mwang’ombe, akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu (Mawasiliano), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Maria Sasabo (katikati), kuzungumza katika kuufunga mkutano wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika, jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Utumishi na Utawala kutoka wizarani, Kitolina Kippa.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la wafanyakazi wa Shirika la Posta, wakimsikiliza Katibu Mkuu (Mawasiliano), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Maria Sasabo, wakati akiufunga mkutano huo. 

Katibu Mkuu (Mawasiliano), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Maria Sasabo akizungumza wakati  akiufunga mkutano wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana. Wengine, kulia ni Kaimu Postamasta Mkuu wa TPC, Hassan Mwang’ombe, kushoto ni Afisa Sheria Eunice Masigati na wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala Kitolina Kippa, wote kutoka wizarani. 
Katibu Mkuu (Mawasiliano), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Maria Sasabo akizungumza katika ufungaji huo. Kulia ni Kaimu Postamasta Mkuu wa TPC, Hassan Mwang’ombe. 
Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la wafanyakazi wa Shirika la Posta, wakifuatilia ufungwaji wa mkutano wao jijini Dar es Salaam jana.
Katibu Mkuu wa TEWUTA Taifa, Junus Ndaro, akitoa salamu za shukurani kwa Katibu Mkuu (Mawasiliano), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Maria Sasabo, mara baada ya hotuba ya kuufunga mkutano huo.
Katibu Mkuu wa TEWUTA Taifa, Junus Ndaro, akitoa salamu za shukurani.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Shirika la Posta Tanzania (TPC), Elia Madulesi, akifafanua jambo wakati wa ufungaji wa mkutano huo.   
Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la wafanyakazi wa Shirika la Posta, wakiwa kwenye ufungaji wa mkutano huo.  
Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la wafanyakazi wa Shirika la Posta, wakifuatilia hotuba ya ufungaji wa mkutano wa baraza hilo, iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu (Mawasiliano), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Maria Sasabo.
Katibu Mkuu (Mawasiliano), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Maria Sasabo (wa tano kutoka kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang’ombe (wa nne mwenye suti nyeusi), pamoja na wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa shirika hilo, mara baada ya kuufunga mkutano huo, jijini jana. 
Katibu Mkuu (Mawasiliano), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Maria Sasabo (wa tano kutoka kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang’ombe (wa tatu kushoto), pamoja na Kamati ya Utendaji ya Baraza Kuu la Wafanyakazi wa shirika la Posta.
Katibu Mkuu (Mawasiliano), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt.Maria Sasabo (wa pili kulia), akizungumza na baadhi ya viongozi wakuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakati akiagana nao mara baada ya kuufunga mkutano wa Baraza Kuu la wafanyakazi wa TPC, ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana. 

No comments