Header Ads

Responsive Ads Here

Mwimbaji Loveness Fungo awatia moyo mashabiki zake

Judith Ferdinand, Mwanza
Mwimbaji Mpya wa nyimbo za  injili Loveness Fungo kutoka jijini Mwanza ametoka na wimbo wa kufunga mwaka 2017 na kuanza mwaka mpya 2018.
Mwimbaji huyo chini ya lebo ya Gospel 255 Entertainment amekuja na wimbo mpya unaoitwa Sio Mwisho kwa ajili ya  kuwatia moyo mashabiki zake mbalimbali.
Akizungumza na BMG, Fungo alisema sababu ya kuimba wimbo huo ni kuwatia moyo wale wote waliopitia na wanaopitia wakati mgumu pamoja na  mambo mazito yakuwakatisha tamaa kwa mwaka mzima.
Fungo alisema, anawatia moyo watu kwa kuwaambia hali na wakati wanaopitia ni ya muda tu, na wala siyo  ya kudumu.
“Kama ni ugonjwa, kukosa kazi, majaribu katika ndoa, biashara kutoenda vizuri kufiwa na wapendwa na mambo mengine mengi ni ya muda tu,  hivyo ninawatia moyo wasione kama mwisho wa maisha yao,” alisema Fungo.
Pia alisema, wimbo huo unawatia moyo na mwaka huu 2018, watambue kuna utukufu  juu yao, ambao unatoka kwa Mungu na utafuta machungu na majonzi yote.

No comments