Header Ads

Responsive Ads Here

MAAFISA UGANI MKOANI DODOMA KUANZA KUPIMWA KAZI ZAO KUPITIA DAFTARI NA SAHIHI ZA WAKULIMA.


Na: Calvin Edward Gwabara
Kondoa- Dodoma

Mkoa wa Dodoma waanzisha daftari maalumu la kujaza kazi wanazozifanya  maafisa ugani  wote mkoani humo ili kuhakikisha kuwa wanatimiza majukumu yao ya kazi ya kutoa huduma za ushauri kwa wakulima kwenye maeneo waliyopangiwa na kuongeza tija.

Muwakilishi wa Afisa kilimo Mkoa wa Dodoama Hadija Kaera akizungumza na wataalamu hao wa kilimo.

Kauli hiyo aimetolewa na muwakilishi wa afisa kilimo Mkoa wa Dodoama Hadija Kaera  wakati akitoa salamu za mkoa kwenye mafunzo ya siku moja kwa wataalamu hao wa kilimo kutoka wilaya nzima ya Kondoa Mkoani Dodoma yaliyoandaliwa na Tume ya taifa ya sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa maendeleo ya Kilimo (OFAB) yenye lengo la kuwajengea uwezo wa matumizi ya bioteknolojia katika kutatua changamoto mbalimbali za wakulima.

Alisema kuwa kumekuwa na malalamiko makubwa kwa wadau wa kilimo hususani wakulima na viongozi wakilalamikia utendaji wa wataalamu hao wa kilimo kutoridhisha na wengne kuonekana kutofanya kazi kabisa wakati wameajiriwa kwa kazi hiyo na wanapata mshahara wa bure bila kufanya kazi waliyokusudiwa kuifanya.


Baadhi ya maafisa ugani hao kutoka wilaya yote ya Kondoa wakifuatilia mafunzo hayo.


”Malalamiko yamekuwa mengi nchi nzima kuwa maafisa ugani kazi zao hazionekane lakini sisi kama mkoa tumeona tuwe na daftari ambalo mataalamu akimhudumia mkulima basi mkulima atatakiwa kusaidia kuwa kweli amehudumiwa kwa kazi iliyoandakikwa ” Alisema Kaera.

“Baada ya kusaidia tumeandaa utaratibu wa kufuatilia kwa mkulima kuona kama kile alichoshauriwa amekitekeleza kama ni kupanda kwa mistari au matumizi ya mbolea na kama atakubali kuwa ameshauuriwa na hakutekeleza pia mkulima atachukuliwa hatua maana amepoteza muda na rasilimali za serikali kwakuwa wataalamu wengine wanaapewa pikipiki na mafuta hivyo mkulima tawajibishwa” Alisisitiza  Kaera.

Alisema kuwa daftari hilo litakuwa ndio suluhisho la kupima utendaji wa wataalamu hao wa kilimo kutokana na kazi wanazozifanya lakini npia itasaidia kuwafanya wale wasiotekeleza majukumu yao kutekeleza maana watabainika kupitia ukaguzi utakaoafanywa na viongozi wa wilaya kupitia utaratibu uliowekwa.
Kaimu Mkurugenzi wa wilaya ya Kondoa ambaye ni afisa kilimo wa wilaya hiyo bwana Hassan Kisseto akizungumza na waandishi wa habari nje ya mafunzo hayo.


Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa wilaya ya Kondoa ambaye ni afisa kilimo wa wilaya hiyo bwana Hassan Kisseto alisema kuwa daftari hilo litaanza kufanya kazi kupitia mashamba darasa hayo ya mfano ya mahindi ya mbegu za mahindi ya WEMA 2109 yaliyoanzishwa na COSTECH kwenye vijiji vilivyochaguliwa kupitia usimamizi wao mzuri ili yaweze kutoa matokeo chanya yatakayowezesha wakulima kuiga mbinu hizo bora zinazofundishwa na wataalamu hao.

Alisema kuwa wakazi wa kondoa wanalima sana mahindi lakini hali ya hewa imekuwa kikwazo kikubwa katika uzalishaji wa zao hilo kwa tija kutokana na kupata mvua zisizokidhi mahitaji ya zao hilo hali mabyo husababisha tija ndogo kwa wakulima kila mwaka.

“Tutahakikisha mashamba darasa haya yanasimamiwa vizuri kwenye kila kijiji ili wakulima wewee kuona umuhimu wa matumizi bora ya mbolea,Kupanda kwa mistari na matumizi ya mbegu bora za kilimo kwa wakulima wa mahindi kwenye wilaya yetu ya Kondoa na kuongeza uzalishaji wa zao hilo kwenye wilaya yetu” Alisema Kisseto.

Akiongea kwa niaba ya wataalamu wenzake wa kilimo  Dwisha Wilson afisa ugani kata ya Kingale alisema kuwa mafunzo hayo yamewasaidia sana kuwakumbusha majukumu yao lakini kuwaongezea ujuzi wa namna ya kutatua changamoto mbalimbali za wakulima kwenye maeneo yao na kuahidi kuzitmia mbinu hizo katika kusaidia wakulima.
Maafisa ugani wa kata na vijiji vyote vya wilaya ya Kondoa  wakiendelea na mafunzo

Alisema kuwa mafunzo hayo yamewapatia mbinu mpya na za kisasa za kiimo ambazo hawakuwa wamezisoma ambazo zimeonekana kusaidia kutatua changamoto nyingi kwa wakulima kwenye nchi mbalimbali na endapo tafiti za kisayansi zinazoendelea zikimalizoka zitasaidia kuongeza tija kubwa kwa wakulima katika mazao mbalimbali nchini.

“Tunashukuru sana COSTECH na OFAB kwa kuona umuhimu wa kutuletea mbinu hizi katika wilaya yetu na kutujengea uwezo tunaahidi kuzitumia na ili zitusaidie kutatua kutatua changamoto mbalimbali za wakulima “ Alisema Wilson.


Baada ya mafunzo hayo kwa maafisa ugani yatafuatia mafunzo kwa wakulima kupitia vikundi na kasha kuanzishwa kwa mashamba darasa ya mahindi kwenye vijiji vilivyochaguliwa na wilaya na kupewa mbegu bora ya mahindi ya WEMA 2109 ambayo yanastahimili ukame ambayo yatapandwa kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo ili wakulima waweze kuona tofauti ya mavuno mashamba darasa hayo na mashamba yao ambayo hawazingatii mbinu hizo.

No comments