Header Ads

Responsive Ads Here

KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATEMBELELEA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO NA MAKUMBUSHO YA OLDUVAI GORGE


 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (kulia) wakizungumza na Mbunge wa viti maalumu, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Zainabu Mwamwindi wakiwa wameongozana na Wajumbe Kamati hiyo wakati walipotembelea jana Jengo la Makumbusho ya Olduvai ya Gorge ambako ni chimbuko la historia ya Binadamu katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) wakiwa na Wajumbe Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakati walipotembelea jana Jengo la makumbusho ya Olduvai ya Gorge ambako ni chimbuko la historia ya Binadamu katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii , Kemilembe Luota ( wa kwanza kushoto) Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Maj. Gen. Gaudence Milanzi (wa pili kulia) wakiwa na baadhi ya Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa kwenye ‘’View Point’ kituo ambacho hutumika kuangalia bonde la Ngorongoro kabla ya kutelemka katika Bonde hilo jana wakati walipofanya ziara ya kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
Huyu ndiye Faru Fausta ni faru kikongwe kuliko wote nchini, akiwa na umri wa miaka 54, na anahitaji matunzo mazuri ili aendelee kuvuta watalii na wanasayansi kutoka kila pembe ya dunia.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Waandishi wa habari wakiji’selfie’ katika banda la Faru Fausta ambaye ndiye faru kikongwe kuliko wote nchini, akiwa na umri wa miaka 54, na anahitaji matunzo mazuri ili aendelee kuvuta watalii na wanasayansi kutoka kila pembe ya dunia wakati walipotembelea banda hilo kwa ajili ya kujionea
Baadhi ya Msururu wa Magari yaliyokuwa yamewbeba wjumbe wa kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii pamoja na viongozi na watumishi wa Wizara pamoja na wa Ngorongoro kwa ajili ya kutelemka kwenyeBonde la Ngorongoro.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiwa katika nje ya ofisi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kuanza ziara.
Kundi la Simba wakiwa wamepumzika walipoonekana jana wakati Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii ilipofanya ziara ya kutembelea Bonde la Ngorongoro.
Bonde la Olduvai Gorge ambako ni chimbuko la historia ya binadamu ni kivutio cha kinachowavuta watalii wengi kutembelea eneo hilo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga( wa kwanza kushoto) akiteta jambo na Wakurugenzi wa Wizara hiyo wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii ilipotembelea jana Makumbusho ya Olduvai GorgeMhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Freddy Manongi akizungumza jana kwenye kikao cha Majumuisho na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii mara baada ya kukamilisha ziara ya kutembelea Bonde la Ngorongoro na Makumbusho ya Olduvai Gorge.(PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA –MALIASILI NA UTALIIKamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kazi nzuri iliyofanya ya ujenzi wa jengo la makumbusho ya kisasa katika Bonde la Olduvai ya Gorge ambako ni chimbuko la historia ya Binadamu.

Kamati hiyo imesema imeridhishwa na ujenzi wa jengo hilo ambalo litawavutia watalii na wanasayansi wabobezi wa masuala ya Malikale kutembelea Makumbusho hiyo.

Kamati hiyo ilibainisha kuwa Makumbusho hiyo mbali ya kutumika kuingiza pesa kupitia watalii pia inatumika kama kielelezo na utambulisho muhimu wa taifa katika kutangaza utamaduni wa Mtanzania ndani na nje ya nchi.

Hayo yalisemwa jana na Kamati hiyo wakati ilipofanya ziara ya kutembelea Ngorongoro Crater na Makumbusho ya Olduvai Gorge katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo. Kemilembe Luota ameipongeza Serikali pamoja na wataalamu kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa kuhakikisha kuwa eneo la Olduvai Gorge linakuwa kivutio bora kwa ajili ya historia ya nchi na kivutio kikubwa cha Utalii duniani.

‘’ Sisi kama Kamati tunaipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kuyafanyia kazi mapendekezo yote tuliyoyatoa kwa mara ya kwanza tulipokuja kwa vile tumeona kazi nzuri imefanyika.’’

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo ametoa wito kwa wananchi kutembelea makumbusho hiyo kwa vile idadi ya watalii wa ndani aliyokutana nayo sio ya kuridhisha.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amesema makumbusho hiyo inatoa ushahidi dhahiri kuwa hata wazungu, mababu zao walitoka Afrika.

Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amesema Makumbusho hiyo hadi hapo ilipofikia imeboreshwa kwa kiwango cha hali ya juu hata hivyo ameitaka Wizara ihakikishe inaitangaza ipasavyo ili watalii wengi zaidi wazidi kutembelea.

Awali, Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka hiyo, FredyManongi amesema tangu kuzinduliwa kwa makumbusho hiyo kwa wiki moja imekuwa ikipokea zaidi ya watalii wapatao 40000 hali inayopekelea kuwa ni miongoni mwa Makumbusho inayofanya vizuri zaidi barani Afrika

No comments