Header Ads

Responsive Ads Here

Watanzania Waguswa na Msamaha wa Rais Magufuli


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli leo Disemba 09,2017 kwenye sherehe za miaka 56 ya Uhuru wa Tanganyika ametoa msamaha kwa wafungwa 8157.
Katika msamaha huo, wafungwa 1828 wataachiwa huru, wafungwa 6329 watapunguziwa muda wao wa kifungo. Pia ametoa msamaha kwa wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa na kuziagiza idara husika kuwatoa leo au kesho.
Kabla ya kutoa hukumu hiyo, Rais Dkt. Magufuli alisema kuwa Tanzania ina wafungwa 39,000 mpaka jana, kati ya hao 37,000 ni wanaume na 2,000 ni wanawake huku wanaosubiri kunyongwa wakiwa ni 522, wanaume 503, wanawake 19 tu.
Wakati huo huo Rais Dkt. Magufuli ametoa msamaha kwa familia ya mwanamuziki Nguza Viking (Babu Seya) na Johnson Nguza (Papii Kocha), ambao walihukumiwa kifungo cha maisha miaka kadhaa iliyopita. Rais Dkt. Magufuli ametoa misamaha hiyo leo katika Sherehe za Maadhimishi ya Miaka 56 ya Uhuru wa Tanganyika yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

No comments