Header Ads

Responsive Ads Here

Urambo Wapokea Huduma za Kisasa Kutoka Duka Jipya la Tigo.

Mgeni rasmi  Katibu Tawala Wilaya  ya Urambo  Bw.Paschal  Byemelwa  akikata  utepe  ikiwa  ni  Uzinduzi wa Duka la Kisasa la Kampuni ya Simu za kiganjani ya Tigo wilayani Urambo katika kutekeleza adhma ya kusogeza karibu huduma za mawasiliano kwa wananchi wilayani humo,Kutoka kulia ni Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Urambo Bi.Margareth Nakainga,wapili kulia ni Meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Bw.Gwamaka Mwakilembe,na wa kwanza kushoto ni Meneja wa Tigo mkoa wa Tabora  Bw.Bright Kisanga.

Duka la kisasa la Huduma kwa Wateja wa Tigo Wilayani Urambo

Mgeni Rasmi  Paschal  Byemelwa,kulia ni Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Urambo Bi.Margareth Nakainga,wapili kutoka  kulia ni Meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Bw.Gwamaka Mwakilembe,na wa kwanza kushoto ni Meneja wa Tigo mkoa wa Tabora  Bw.Bright Kisanga wakipiga makofi kushangilia tukio la kutaka utepe kama ishara ya Uzinduzi wa Duka hilo la Kisasa wilayani Urambo.

Picha ya pamoja baada ya Uzinduzi wa Duka hilo
Mmoja kati ya maafisa wa Tigo  Bi.Tunu Kazinja  akitoa maelezo kwa huduma ambazo wanazitoa mara baada ya uzinduzi wa Duka hilo la Kisasa wilayani Urambo.

Mgeni Rasmi  Katibu Tawala wilaya ya Urambo Paschal Byemelwa pamoja na wageni wengine waalikwa katika hafla fupi ya uzinduzi wa Duka hilo la kisasa,walipata fursa ya kuangalia bidhaa mbalimbali za Tigo ambazo zilikuwa zikioneshwa nje ya Duka hilo la Kisasa.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Urambo wakipata maelezo ya huduma zinazotolewa na Kampuni ya Tigo katika moja ya Banda la maonesho wakati wa hafla fupi ya Uzinduzi wa duka la Kisasa wilayani Urambo.

Katibu Tawala wilaya ya Urambo Bw.Paschal Byemelwa akihutubia wakati wa Uzinduzi wa duka la Tigo  wilayani Urambo ambapo ameishukuru kampuni ya Tigo kwa kufungua Duka hilo la Kisasa ambalo amesema litasaidia kuwapunguzia adha kubwa wananchi wa Urambo ambao walikuwa wanalazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma. 
Baadhi ya wananchi wa Urambo wakimsikiliza katibu tawala wilaya ya Urambo Bw.Paschal Byemelwa wakati akiwahutubia katika hafla fupi ya uzinduzi wa duka hilo la kisasa.
Meneja wa kanda ya ziwa wa Tigo Bw.Gwamaka Mwakilembe akizungumza na wananchi wa Urambo wakati wa uzinduzi wa Duka la kisasa wilayani humo ambapo alieleza kuwa kampuni ya Tigo  ambayo inaongoza kwa mageuzi ya kidigital nchini imeamua kuzindua duka hilo ikiwa ni muendelezo wa juhudi zake kuboresha huduma kwa wateja wake.


Urambo, 12 Desemba, 2017- Katika mwendelezo wa harakati za kuhakikisha kuwa wateja wake wote wanapata huduma bora kwa urahisi, kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali Tigo Tanzania leo imezindua duka kubwa la kisasa wilayani Urambo katika Mkoa wa Tabora.


Duka hilo jipya linapatikana katika mtaa wa Nsanjo, mkabala na depot ya Pepsi katika mji wa Urambo, lina uwezo wa kuwahudumia wateja zaidi ya 580,000 wa Tigo wanaopatikana wilayani hapo na viunga vyake.


Akizungumza katika hafla fupi ya kuzindua duka hilo jipya la Tigo, Meneja wa Eneo la Ziwa wa Tigo, Gwamaka Mwakilembe alisema kuwa ufunguzi wa duka hilo jipya unaendana na mpango wa upanuzi na ukuaji wa kampuni hiyo ya simu unaolenga kuongeza idadi ya vituo vya huduma kwa wateja huku ikihakikisha kuwa bidhaa na huduma zote zinapatikana kwa urahisi na wateja wake nchi nzima.


‘Tigo imejizatiti kufanya uwekezaji utakaohakikisha wateja wetu wanapata huduma kwa viwango vya kimataifa ili waweze kupata suluhisho muafaka kwa mahitaji yao. Ufunguzi wa duka hili la kisasa mjini Urambo kunafanya idadi ya maduka yetu ya Tigo kufikia 15 katika Ukanda huu wa Ziwa, huku jumla ya maduka yetu yote ya Tigo nchini ikifikia 75,’ alisema.


‘Uzinduzi huu unaendana na sifa kuu ya Tigo kuwa mtandao unaowaelewa zaidi wateja wake na kuwapa bidhaa na huduma bora, za kibunifu, zinazoendana na mahitaji yao. Tunaendelea kuwekeza katika upanuzi na uboreshaji wa mtandao wetu wa simu, ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anakuwa sehemu ya mabadiliko na faida za ulimwengu wa kidigitali unaoongozwa na Tigo,’ Mwakilembe alifafanua.

Kwa upande wao, wakaazi wa Urambo wameelezea kufurahishwa kwao na ujio wa duka hilo jipya la Tigo kwani litawapunguzia adha ya kusafiri kwa mwendo mrefu kupata ufumbuzi wa matatizo yao ya simu pamoja na kuboresha upatikanaji wa huduma za simu katika wilaya hiyo.


No comments