Header Ads

Responsive Ads Here

ULEGA ASHUHUDIA UCHOMWAJI WA ZANA HARAMU ZA UVUVI MKOANI KIGOMA
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akishuhudia uteketezaji wa zana haramu za uvuvi katka Ziwa Tanganyika katika kijiji cha Buhingu mkoa wa Kigoma.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na viongozi mbalimbali na wananchi kijiji cha Buhingu mkoa wa Kigoma.Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akimkabidhi cheti ndugu Mapango Thomas cha utambuzi ili waweze kusimamia ipasavyo rasilimali za uvuviMkuu wa Wilaya ya Uviza,Mwavua Mrindo akizungumza na wananchi na viongozi mabli mbali katika kijiji cha Buhingu mkoa wa Kigoma.Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwa ameongoza na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Kingoma wakivuka mto Malangalasi kuelekea katika kijiji cha Buhingu wilayani Uviza Kigoma.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii Kigoma. Kufuatia Wimbi la Uvuvi haramu nchini,Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalla Hamisi Ulega janao ameshuhudia uchomwaji wa zana haramu za Uvuvi katika Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, kijiji cha Buhingu mkoani Kigoma.

Mwenyekiti wa kikundi cha Usimamizi shirikishi rasilimali za Uvuvi (BMUs) katika Kijiji cha Buhingu Bw.Richard Nkayamba amemweleza naibu Waziri kuwa kazi yao kubwa ni kuhakikisha wanakomesha Uvuvi haramu katika Kijiji cha Buhingu na kuweka mazingira safi.

"Kwa kiasi kikubwa tumedhibiti  Uvuvi haramu pamoja na kutoa elimu kwa Jamii za Wavuvi, kuhusu Umuhimu wa Uvuvi endelevu kwa kushirikiana na vikundi vya Ulinzi shirikishi BMUs 21 pamoja na shirika lisilokuwa la kiserikali la Tuungane lililopo katika kijiji cha Buhingu"alisema Nkayamba

Aliongeza,"Tunakamata nyavu haramu bila kujali ni za nani,na hii inatujengea chuki kwa wamiliki wa Nyavu husika"Akiongea na uongozi wa Halmashauri ya Uvinza pamoja na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo,Ulega amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Uvinza kuona ni namna gani wanaweza kuziwezesha BMUs zilizopo kijijini hapo.

"Naombeni sana mziwezeshe hizi BMUs wapeni tenda za kukusanya Maduhuri ya Samaki kwa Wavuvi hawa ili hizi BMUs ziweze kujiendesha zenyewe"Mhe.Ulega alisisitiza kuwa kama wakipewa BMUs kukusanya Maduhuri basi watakuwa wametengeneza ajira kwa Vijana hao.VileVile aliwaasa sana BMUs kuwa Waadilifu ili waweze kuaminiwa"

Katika hatua nyingine Mhe.Ulega aliwatunuku vyeti vya Utambuzi baadhi ya BMUs waliokidhi sifa za kusimamia rasilimali za Uvuvi katika ziwa hilo.Awali Mhe Ulega alikemea vikali asasi za Kiraia kujiingiza katika kushabikia siasa badala ya kufanya kazi za kuelimisha Umma.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bi.Mwanamvua Mrindo amesema kuwa amefarijika sana kwa ujio kwa Mhe.Naibu waziri katika Wilaya ya Uvinza ili kutatua Changamoto zinazowakabili.

Baadhi ya wananchi waliokuwa wakimsubiri mhe.Ulega katika kijiji cha Mgambo,walimweleza kero zao ikiwa ni pamoja na uingizwaji ovyo Mifugo katika kijiji cha chao.Naibu waziri amemwagiza MKUU wa Wilaya ya Uvinza kushughulikia kero hizo.

No comments