Header Ads

Responsive Ads Here

TIGO YATOA MAMILIONI KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA MSIMU WA SIKUKUU

Afisa Vigezo wa Tigo, Abdallah Nguba (kushoto) pamoja na Meneja wa Wateja wa Tigo Mary Rutta (kati) wakifanya droo ya kuwapata washindi wa promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na ushinde,' ambapo wateja wa Tigo wanapata fursa ya kushinda hadi milioni 15 kila wanapotumia Tigo Pesa. Jumla ya wateja 20 walijishindia kati ya shilingi laki tano na milioni moja leo. Kulia ni Afisa wa Bodi ya Michezo ya Bahati na Sibu Tanzania, Jehud Ngolo. 

Meneja wa Wateja wa Tigo Mary Rutta (kulia) akiwatangaza washindi wa  wa promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na ushinde,' ambapo wateja wa Tigo wanapata fursa ya kushinda hadi milioni 15 kila wanapotumia Tigo Pesa. Jumla ya wateja 20 walijishindia kati ya shilingi laki tano na milioni moja leo. Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael

Mojawapo ya washindi wa promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na ushinde,', Saidi Khatib Kiko, mkaazi wa Kimara akionesha sura ya furaha ya ushindi wakati wa hafla ya kukabidhiwa zawadi iliyofanyika katika ofisi za Tigo jijini Dar es salaam leo. Saidi alikuwa mojawapo ya washindi 20 waliojinyakulia kati ya shilingi laki tano na shilingi milioni moja katika promosheni hiyo ambapo wateja wa Tigo Pesa wana nafasi ya kujishindia hadi shilingi milioni 15.   Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto) akiwatangaza washindi wa  wa promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na ushinde,' ambapo wateja wa Tigo wanapata fursa ya kushinda hadi milioni 15 kila wanapotumia Tigo Pesa. Jumla ya wateja 20 walijishindia kati ya shilingi laki tano na milioni moja leo. Kulia ni Meneja wa Wateja wa Tigo, Mary Rutta.
  • Wateja 20 wapokea zawadi kemkem za pesa kwa kufanya miamala kupitia Tigo Pesa


Dar es Salaam, 8 Novemba, 2017- Huduma ya kutuma na kupokea fedha inayoongoza nchini Tanzania, Tigo Pesa leo imewatangaza na kuwazawadia washindi 20 wa promosheni yake ya ‘Tumia Tigo Pesa na Ushinde,’ inayoendelea katika msimu huu wa Krismasi na Mwaka mpya ambapo wateja wanajishindia mamilioni ya pesa.


Washindi wanne (4) wamepata bahatiya kushinda zawadi za kila siku za shilingi milioni moja kila mmoja, huku wengine 16 wakijaza mifuko yao na donge nono la shilingi laki tano (TZS 500,000) kila mmoja.  each. Jumla ya shilingi milioni 12 zimetolewa kama zawadi kwa wiki  hii.


Washindi wa zawadi za TZS 1 milioni ni wafanyabiashara Neema Fredrick Mosha, Fredrick Joseli Mponzi , Sefu Athumani Sefu na Hadija Mohamed Lukulumbale ambaye ni mama nitilie.


Washindi  wa zawadi za TZS 500,000 ni Michael Joseph Moshi, Moses Muhonga Amuli, Saidi Khatib Kiko, Sylvester Michael Madaga, Aziza Ramadhani Ngozi, Evelyne Gwamaka Mwakyembe, Tumsifu Harold Temu na Sikudhani Constantine Mwenda. Wengine walioshinda TZS 500,000 ni Queentina Msafiri Mbwambo, Hilary Andrew Massawe, Ashura Ally Salim, Halima Saidi Shaabani, Fatuma Ally Makumbo, Halima Saidi Sangiwa, Jenifer Samuel Apolinale na James John Mkanula.


‘Tunatarajia kupata jumla ya washindi 153 katika kipindi cha mwezi mmoja wa promosheni hii. Bado tuna zawadi za thamani ya TZS 108 milioni kutoa kwa washindi 133,’ Meneja wa Wateja wa Tigo, Mary Rutta alisema wakati akikabidi zawadi kwa washindi Dar es Salaam leo.


Alibainisha kuwa pamoja na zawadi za kila siku, promosheni hiyo ya ‘Tumia Tigo Pesa na Ushinde,’  itakuwa na zawadi kubwa za mwezi  TZS 15 milioni, TZS 10 milioni na TZS 5 milioni.


‘Kushiriki katika promosheni hii ni rahisi na ni wazi kwa wateja wote wa Tigo Pesa ambao wanahitaji kutumia huduma ya Tigo Pesa kwenye simu zao ili kupata nafasi ya kushinda. Kadri unavyotumia huduma ya Tigo Pesa ndivyo unavyojiongezea nafasi ya kushinda,’ alisema.


Tigo Pesa inajivunia kufanya miamala ya zaidi ya TZS 1.7bn kila mwezi kupitia mtandao wake mpana wa mawakala zaidi ya  70,000 waliosambaa nchini kote.  

                                                                                 

No comments