Header Ads

Responsive Ads Here

TANESCO yakabidhiwa tuzo ya Utunzaji Bora wa Mahesabu Kwa Mwaka 2016/2017

Shirika la Umeme nchini (TANESCO) limekabidhiwa tuzo ya Utunzaji bora wa Mahesabu na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA), baada ya kufanya Vizuri kwenye kada hiyo katika Mwaka wa fedha 2016/2017.
Akipokea tuzo hiyo Afisa mkuu wa Masuala ya fedha wa TANESCO, Bi RENATA NDEGE ameishukuru Bodi ya Wahasibu na wakaguzi (NBAA), kwa kutambua Utendaji Kazi wa Shirika hilo la Ugavi wa umeme hapa Nchini.
" Napenda kuishukuru Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi kwa kuonesha imani katika Utendaji kazi wetu hususani kwenye Kada hii ya Masuala ya Utunzaji wa fedha, Sisi kama Idara tunaahidi Kuimarisha Utendaji Kazi wa TANESCO kwa Kushirikiana na NBAA" alisema Bi RENATA.
Baadhi ya Watumishi wa Idara ya Fedha katika Shirika la Umeme (TANESCO), wakionekana kufurahia tuzo waliyokabidhiwa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu, wameuambia Mtandao wa www.habari360.co.tz kwamba Wataendelea Kuchapa kazi Kwa weledi ili Kulisaidia Shirika Kutimiza Majukumu yake kwa Umma wa Watanzania.
Tuzo hiyo iliyokabidhiwa kwa Idara ya Fedha ya Shirika la Umeme (TANESCO), imeakisi Ubora wa Shirika hilo la Umma katika Utunzaji wa Mahesabu ya Fedha.
Afisa mkuu wa Masuala ya fedha wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Bi RENATA NDEGE akizungumza na Waandishi wa habari (Hawapo pichani), mara baada ya Kupokea tuzo ya utunzaji Bora wa Mahesabu kutoka Bodi ya wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu (NBAA) katika mwaka wa fedha 2016/2017, Sherehe hizo Zimefanyika Jijini Dar es Saalam.
Afisa mkuu wa Masuala ya fedha wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Bi RENATA NDEGE, akionesha tuzo ya utunzaji Bora wa Mahesabu aliyokabidhiwa na Bodi ya wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu (NBAA) kwa niaba ya Shirika la umeme, Baada kufanya vizuri kwenye kada ya utunzaji Mahesabu ya fedha kwa Mwaka 2016/2017.
Afisa mkuu wa Masuala ya fedha wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Bi RENATA NDEGE, akiwa kwenye picha ya pamoja na Baadhi ya watumishi katika Idara ya Uhasibu Mara baada ya Kukabidhiwa tuzo ya Utunzaji Bora wa Mahesabu katika Mwaka wa fedha 2016/2017.
Watumishi katika Idara ya Uhasibu Kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), wakifurahia tuzo ya Utunzaji Bora wa Mahesabu BAada ya Kukabidhiwa na Bodi ya Wahasibu na wakaguzi wa Mahesabu (NBAA), Sherehe hizo zimefanyika Jijini Dar es Salaam.

No comments