Header Ads

Responsive Ads Here

SBL yazindua Vodka mpya - SMIRNOFF X1 Extra Pure Vodka

 Wadau wakionesha chupa yenye kinywaji kipya cha Smirnoff X1 Extra Pure Vodka wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika Ukumbi wa LAPF Kijitonyama jijini Dar es Salaam jana.
 Meneja Ubunifu wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Wankiyo Marando akieleaea kinywaji hicho na ubora wake.
 Mtaalamu wa kuchanganya vinywaji, Junior Charles akielekeza namna ya kuchanganya kinywaji hicho.
 Mafuriko ya wadau katika uzinduzi wa kinywaji hicho uliofanyika Ukumbo wa LAPF Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
 Warembo wakiwa na kinywaji hicho kabla ya kwenda kupeleka kwa wadau
 Chupa ya kinywaji hicho ikiwa imeinuliwa juu na wadau.
 Mmoja wa wadau akiangalia chupa yenye kinywaji hicho.
 Uzinduzi ukiendelea.
 Wadau wakiwa kwenye hafla hiyo
 Muonekano wa kinywaji hicho katika chupa.
 Hapa ni furaha tupu katika hafla hiyo
 Wadau wakigonganisha glasi wakati wa uzinduzi huo.
Wadau mbalimbali wakifurahia kichwaji hicho huku wakiburudika kwa muziki.


Kampuni ya Bia ya Serengeti, SBL imetangaza uzinduzi wa vodka mpya yenye chapa ya
Kitanzania iitwayo SMIRNOFF® X1, Xtra Pure vodka.

Akizungumza katika uzinduzi wa kinywaji hicho jijini Dar es Salaam jana, Meneja
Ubunifu wa SBL, Wankiyo Marando alisema uzinduzi huo ni mwendelezo wa bidhaa ya
chapa maarufu iliyopo sokoni kwa sasa ya SMIRNOFF® No.21 ambayo wateja wa SBL
wamekuwa wakiifurahia kwa muda sasa hapa nchini.

Alisema kinywaji hicho chenye ubora wa hali ya juu kilichochakatwa mara tatu zaidi
kinakuja na ujazo wa kilevi (ABV) wa 43%, huwa na ladha ya kupendeza kwa kunywa
ama kwa kuchanganya na kinywaji kingine au hivyo hivyo bila kuchanganywa na
imetengenezwa kwa unywaji wa matukio yote.

“Kinywaji kipya cha SMIRNOFFX1 Extra Pure Vodka ni bidhaa bora ya uhakika na ya
kufurahiwa hasa tunapokaribia msimu wa sikukuu lakini tunawasisitizia watumiaji
wote  wanywe kistaarabu,” alisema Marando.

“Kuanzia siku za mapumziko, midundo ya nguvu ya ngoma kwenye muziki mpaka sherehe
za nyama choma, kuna fursa nyingi sana ambazo wateja wetu wanaweza kufurahia
utamaduni na muunganiko wetu wa Kitanzania- kuwaleta watu wetu wa tamaduni na
desturi zote kwa pamoja kwakuwa nyakati hufanywa maridhawa ikiwa kila mmoja
anajumuika,” Marando alisema hayo akisisitiza kuwa katika nyakati kama hizo,
SMIRNOFF X1 Xtra Pure ni kitu sahihi kabisa cha kuwaleta watu pamoja.

Alisema kuwa SMIRNOFF X1 Xtra Pure Vodka ambayo iko kwenye ujazo wa chupa ya 750ML
na 200ML itapatikana katika maduka vyote vya mauzo ya pombe kwa bei pendekezwa ya
rejareja ya shilingi za Kitanzania 12,000 (750ML) na shilingi za Kitanzania 4,000
(200ML).

Kwa uzinduzi huu mpya wa ujazo imara, wateja wa SBL sasa wataweza kufurahia chapa
ya vodka kwa bei thabiti ambayo ni sehemu ya chapa ya kimataifa ya SMIRNOFF®.
Kama moja ya chapa ya Vodka iliyotunukiwa tuzo nyingi zaidi duniani, SMIRNOFF®,

imekuwa ikitambulika siku zote kwa ubora wake na imekuwa ikinywewa kistaarabu kwa
zaidi ya nchi 130 duniani.

No comments