Header Ads

Responsive Ads Here

Picha : SHIRIKA LA KIVULINI LAFANYA KIKAO CHA WANA MABADILIKO MRADI WA USAWA WA KIJINSIA KUJENGA UCHUMI KWA WANAWAKE NA VIJANA SHINYANGAKatika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na watoto,Shirika la Kivulini limefanya kikao cha wana mabadiliko kwa ajili ya kufanya tathmini na mrejesho wa shughuli za mradi wa usawa wa kijinsia kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake na vijana unaotekelezwa halmashauri wilaya mbili za Shinyanga na Kishapu mkoani Shinyanga.

Kikao hicho kilichokutanisha wana mabadiliko 65 kutoka vijiji vitano vya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (Shinyanga Vijijini) ambavyo ni Nyida,Nsalala,Butini,Nduguti na Welezo kimefanyika leo Disemba 5,2017 katika Ukumbi wa mikutano wa Empire Hotel mjini Shinyanga.

Akizungumza katika kikao hicho, Afisa mwandamizi wa mradi huo, Bi. Eunice Mayengela alisema lengo la kikao hicho ni kujadili mafanikio na changamoto ambazo wana mabadiliko wanakutana nazo kwenye maeneo yao katika kutekeleza mradi.

Mayengela alisema suala ya ukatili dhidi ya wanawake ni la jamii nzima hivyo panahitajika ushirikiano wa pamoja ili kuhakikisha vitendo hivyo vinatoweka katika jamii.

“Lazima tushirikiane kwa pamoja kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto,wana mabadiliko,serikali na wadau wengine tunapaswa kuungana ili tuwe na nguvu ya pamoja”,aliongeza Mayengela.

Mayengela alitumia fursa hiyo kuwataka wanawake kuacha uoga wanapofanyiwa vitendo vya kikatili ikiwemo kubakwa na badala yake watoe taarifa kwenye vyombo vya sheria ili kukomesha vitendo hivyo katika jamii.

Naye afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Masili Mhoja aliwataka wanawake kupaza sauti wanapofanyiwa ukatili.

“Akina mama pazeni sauti,fuateni sheria,msiwahurumie sana hawa wanaume,nanyi wanaume acheni mila na desturi zilizopitwa na wakati,wapeni urithi wa mali ikiwemo ardhi wake zenu,hata kupigana katika ndoa nako kumeshapitwa na wakati”,alieleza Mhoja.

Mhoja pia alikemea tabia ya akina baba kuwapa ujauzito watoto badala ya kuwaacha wasome kwa ajili ya kuwasaidia katika maisha yao.

Mhoja aliwataka wana mabadiliko kutumia vyema fursa waliyopewa na shirika la Kivulini ambalo limekuwa likiwapatia ujuzi na mbinu mbalimbali katika kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Kwa upande wao washiriki wa kikao hicho walisema wamekuwa wakitoa elimu kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia kwa jamii,kutatua migogoro ya ndoa na ardhi.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA KIKAO HICHO
Afisa mwandamizi wa mradi wa usawa wa kijinsia kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake na vijana, Eunice Mayengela akizungumza katika kikao cha wana mabadiliko kwa ajili ya kufanya kutathmini na mrejesho wa shughuli za mradi- Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Afisa mwandamizi wa mradi wa usawa wa kijinsia kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake na vijana, Eunice Mayengela akizungumza katika kikao hicho ambapo aliwataka wana mabadiliko kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii. 
Mayengela akisisitiza umuhimu wa wadau wote kushirikiana ili kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Wana mabadiliko wakimsikiliza afisa mradi wa usawa wa Kijinsia kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake na vijana kutoka Shirika la Kivulini, Eunice Mayengela.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Masili Mhoja akizungumza katika kikao hicho ambapo aliitaka jamii kubadilika na kuachana na mila na desturi zilizopitwa na wakati zinazogandamiza wanawake na watoto.
Wana mabadiliko wakiwa ukumbini.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Masili Mhoja akisisitiza umuhimu wa wanandoa kupendana kama njia mojawapo ya kukabiliana na ukatili katika familia.
Kikao kinaendelea...
Wana mabadiliko wakifuatilia kwa makini kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Afisa miradi shirika la Kivulini,Glory Mlaki  akizungumza wakati wa kikao hicho
Wana mabadiliko wakiwa ukumbini
Kulia ni Afisa mwandamizi wa mradi wa usawa wa kijinsia kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake na vijana, Eunice Mayengela na Afisa Mwandamizi msaidizi wa mradi huo,Vaileth Elisa wakiwa ukumbini
Kulia ni Afisa miradi shirika la Kivulini,Glory Mlaki  akitoa mwongozo namna ya kufanya kazi ya vikundi wakati wa kikao hicho cha tathmini na mrejesho wa shughuli za mradi wa usawa wa kijinsia kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake na vijana 
Kulia ni Afisa mwandamizi msaidizi wa mradi wa usawa wa kijinsia kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake na vijanaVaileth Elisa kutoka shirika la Kivulini akimsikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa washiriki wa kikao hicho wakati wa kazi za makundi.
Kazi za makundi zikiendelea...
Wana mabadiliko wakifanya kazi ya kundi lao
Mwana mabadiliko Mwendwa Yasin kutoka kijiji cha Welezo akiwasilisha kazi ya kundi lake kuhusu shughuli mbalimbali wanazofanya katika kutekeleza mradi wa 
Mwana mabadiliko Monica Simon akichangia hoja wakati wa kikao hicho
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

No comments