Header Ads

Responsive Ads Here

Mshindi wa Mamilioni ya Tatu Mzuka apeleka Neema wilayani Ukerewe

Judith Ferdinand, Mwanza
Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza imepokea msaada wa mabati bando 18, kwa ajili ya  ujenzi wa zahanati ya Murutunguru.
Msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni tano ambayo ni mabati 216, umetolewa na kampuni ya mchezo wa kubahatisha Tatu Mzuka, mara baada ya mshindi  wa droo ya  jumapili iliyopita kutoka Mwanza ambaye ni Simon Matto mkazi wa Bugando Jijini Mwanza.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi mabati hayo sambamba na hundi kwa mshindi, iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Afisa Uhusiano wa  Tatu Mzuka Kemi Mutahaba alisema wanayofuraha kumpata mshindi huyo ambaye ni kwa mara ya kwanza kwa mkoa wa  Mwanza kupatikana tangu kuanza kwa mchezo huo uanzishwe.
Mutahaba alisema baada ya miezi miwili tangu kuanzishwa kwa mchezo huo wa bahati nasibu nchini, wamekuwa na utaratibu  wakutoa msaada kwa jamii anayotoka mshindi wa droo ya kila wiki hivyo mabati hayo ni moja wapo ya kutekeleza.
Alisema baada ya kujadiliana waliamua kupeleka msaada huo katika zahanati Murutunguru wilayani Ukerewe ambacho kimeisha anza kujengwa na wataezeka kwa kutumia mabati hayo.
Pia alisema mbali na mabati hayo kampuni yao imeshatoa milioni 100  kwa Wizara ya Mazingira nchini,msaada wa  matofali  katika shule mkoani Dodoma pamoja na madawati na vitabu shule za mkoani Dar es salaam, ambapo kwenye msaada wa jamii wanatoa vitu na mshindi anapatiwa pesa taslimu.
Hata hivyo alisema wanamwanza wanatakiwa kucheza mchezo huo,kwani ni wakweli na mshindi anapatikana kiuwalali bila upendeleo.
Kwa upande wake mshindi wa mchezo huo Simon Matto alisema, amekuwa mshiriki wa tatu mzuka na hatimaye ameibuka na ushindi na kujinyakulia kitita  cha milioni 18, fedha ambazo zitamsaidia kujiinua katika shughuli zake,hivyo aliwaomba watanzani kushiriki kucheza kwani unakuwa umewekeza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe Frank Bahati, aliipongeza  tatu mzuka  na kwani bahati nasibu yao haiishi kujali washindi bali na jamii inayowazunguka,hivyo msaada huo umekuja wakati muafaka,  maana wilaya hiyo inavituo 28, lakini Murutunguru ndio kilikua na uhitaji zaidi na mabati hayo yataenda kusaidia kituo hicho ambacho kinaenda kupandishwa hadhi na kupitia msaada ndoto itatimia.
Bahati alisema, makampuni mengine nayo yaige,pia yasiangalie kunufaisha wachache bali jamii mzima pamoja na kuwezesha washiriki kujikwamua.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Joshua Monge alisema, anaishukuru  Tatu Mzuka kwa msaada huo, kwani sekta ya afya inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo serikali pekee haiwezi kumaliza, hivyo mabati hayo yatatumika kuezekea zahanati ya  Murutunguru ikiwemo jengo la afya ya mama na mtoto na maabara.
Aidha Diwani wa Kata ya Murutunguru Mwl. Nicholas Mnyoro alisema, mabati hayo yanaenda kusaidia kituo hicho cha afya, ambacho kilikua kinahudumia  takribani watu 8000,pia jambo hilo litasaidia wananchi kuiamini Tatu Mzuka na kuendelea kujitoa hill kuharakisha ujenzi wa kituo hicho.

No comments