Header Ads

Responsive Ads Here

MAZISHI WA MWANDISHI MKONGWE MAYAGE S MAYAGE


Mayage S.Mayage kuzikwa Mbweni Jijini Dar Alhamis

MWANDISHI wa habari mwandamizi, Mayage Mayage, (56), amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda.

Mayage amekutwa na umauti katika Hospitali ya Misheni ya Mbweni, Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa kwa muda wa wiki mbili.Taarifa kutoka kwa mdogo wake Emmanuel Mayage, alisema kuwa madaktari waligundua kaka yake kuugua saratani na kifua kikuu (TB).

Emmanuel alisema kuwa Mayage atazikwa Alhamis Desemba 28, 2017 katika makaburi ya Mbweni, eneo linaloitwa Maputo.Taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani kwa marehemu Mbweni Kijijini, eneo la Maputo ambako ndugu na jamaa wanakutana.

“Mayage aligundulika kuwa na saratani mwaka mmoja uliopita na alianza matibabu katika hospitali mbalimbali nchini ikiwemo Ocean Road na Muhimbili.

Alisema hali yake iliimarika kwa muda, lakini ikabadilika wiki tatu zilizopita na kusababisha kulazwa katika hospitali ya Mbweni.Emmanuel alisema kuwa akiwa hospitalini hapo, kaka yake aligundulika pia kuwa na maradhi ya kifua kikuu na alianzishiwa tiba.

Mayage alianza kazi za uandishi wa habari mwaka 1995, akifanya kazi katika kampuni ya magazeti ya Habari Corporation; inayochapisha magazeti ya Mtanzania, RAI, Dimba, The African na Bingwa.Baadaye Mayage aliondoka katika magazeti hayo na kuanza kazi ya uandishi wa habari wa kujitegemea, yeye akijiita “mwandishi huru.”

Akiwa mwandishi huru, Mayage alikuwa akiandikia magazeti mbalimbali nchini, yakiwemo ya Raia Tanzania, MwanaHalisi na mpaka kufariki kwake alikuwa mwajiriwa wa gazeti la TAZAMA.

Salva Rweyemamu, aliyekuwa mhariri mtendaji wa magazeti ya Habari Corporation amemzungumzia Mayage na kueleza kuwa alikuwa mwandishi mzuri, mahiri, asiyeogopa na aliyefanya kazi yake kwa weledi, huku akiwa mchambuzi mzuri wa habari za siasa za nchi hii.

“Mayage hakushindwa kazi yoyote aliyotumwa, ukimwagiza lazima uwe na uhakika wa kuifanikisha, hakika tumepoteza mchapakazi,” alisema Salva kwa masikitiko

NAMNA YA KUFIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU.

Ramani ya msiba

Msiba uko nyumbani kwake Mbweni Kijijini, Dar es Salaam, eneo la Mbweni Maputo,siyo mbali na hospitali ya Mbweni Misheni.

Ukiwa unatokea Mwenge unapanda daladala ziendazo Mbweni, unashukia kituo cha Mbweni Misheni, kisha hatua chache mbele kuna njia inayokwenda kushoto ituate hiyo.Ifuate barabara hiyo kwa kuongozwa vibao vinavyoelekeza kuelekeza msiba ulipo mpaka utakapofika nyumbani kwa marehemu, ambaye ni maarufu kama Mzee wa Magazeti.

Njia nyingine ni kupanda mabasi ya Makumbusho-Bunju/Magamoyo, shukia  kituo cha Mianzini Bunju.
Hapo chukua bodaboda kwa gharama ya 3000/= hivi hadi mbele kidogo ya Mbweni Misheni Hospitali.Hapo kata kushoto na muelekeze bodaboda afuate vibao vya kuelekeza msiba hadi nyumbani kwa marehemu.

Kwa wenye usafiri binfsi; unaweza kufika kwa njia mbili:

1.Ukitoka Mwenge nenda mpaka Petrol Station ya Lake Oil eneo la Bunju.Hapo kuna barabara ya lami kuelekea Mbweni.Ifuate hadi Mbweni Misheni Hospitali.Baada ya hapo kata kushoto.Fuata vibao vya msiba.

2.Ukitoka Mwenge nenda hadi njia panda Mbweni,fuata njia ya daladala, pita mageti ya Jeshi hadi Mbweni Kijijini.Endelea mbele hadi Mbweni Misheni Hospitali.Sogea mbele kidogo, halafu kata kushoto na anza kufuata maelekezo ya vibao vya msiba.

No comments