Header Ads

Responsive Ads Here

Kwamba Vyama vya upinzani ni sawa na Magonjwa ya Mlipuko

Na Katumba K.Madua
Mambo vipi mtu wangu unayesoma makala yangu muda huu. Mwaka 1992 nchi yetu iliingia kwenye mfumo wa  vyama vingi mfumo ambao ulikuwepo kabla ya uhuru.
Chama cha Mapinduzi ni kuungana kwa vyama vya  TANU na ASP. Hiyo ilikuwa ni tarehe 5-2-1977. Nini basi maudhui ya andiko langu? Nchi ya Tanzania na CCM ni kama mwili wa binadamu. Mwili wa binadamu hata uwe mkubwa kiasi gani lakini kuna magonjwa ya mlipuko yakiingia ama kwa hakika mwili lazima uteteleke.
Hivyo napenda kusema kuwa vyama vya upinzani hapa nchini ni sawa tu na magonjwa ya mlipuko na yakipata tiba hutoweka. Magonjwa ya mlipuko huwa na tabia ya kuwaogopesha jamii husika hadi za kimataifa ama kwa hakika nchi husika isipopambana na mlipuko huo maafa hutokea mengi.
Napenda kusema wale wanaCCM wote waliohama na kwenda vyama vingine tunasema wamekufa na magonjwa ya mlipuko. Moja ya magonjwa ya mlipuko kwa vyama hapa Tanzania ni kama Chadema, ACT, CUF, NCCR, TLP nk.
Sasa msomaji wangu nakupa hii.
1.Chadema -kipundupindu
2.CUF-kichocho
3.ACT-Mafua
4.TLP -Surua
5.NCCR-Mafua ya  ndege
6.Chauma-Homa ya bonde la UFA.
Sasa jiulize hapo kuna ugonjwa wa kumsumbua binadamu wakati tayari kuna chanjo na tiba yake. Hivyo wanaccm kazi ni kupambana na magonjwa ya mlipuko ambayo kamayanatokea ndani ya chama lazima baadhi ya watu watakufa aidha kwa uzembe au kwa kuchelewa kupata dawa husika.
Viongozi wa chama cha mapinduzi ambao mmechaguliwa kwenye chaguzi zilizopita.Nawaomba sana mhakikishe hayo magonjwa ya mlipuko yanapata tiba stahiki ili yasije kuwadhuru wanachama wetu, kumbuka CCM ndiyo mwili hivyo viongozi ulindeni mwili kupambana na magonjwa ya mlipuko.
Kidumu Chama cha Mapinduzi.

No comments