Header Ads

Responsive Ads Here

GAUDENTIA KABAKA ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA WA UWT

Mhe. Gaudensia Kabaka Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Wanawake Tanzania 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya wadhamini wa UWT akihutubia wakati wa kufunga mkutano mkuu wa tisa wa UWT uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi waliochaguliwa kuongoza kwa kuzingatia Katiba, Kanuni  za UWT, CCM na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kuhitimisha Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Jakaya Kikwete.
Makamu wa Rais aliwasihi viongozi hao kuvunja makundi ya kampeni nwaliyokuwa nayo na kujenga Umoja na Mshikamano ndani ya Jumuiya na Chama.
Makamu wa Rais  alisisitiza kufanya kazi kwa umoja, mshikamano na kwa uzalendo “Kushinda kuwa Kiongozi haina maana unajua yote, tuwe tayari kukosoana lakini tusisingiziane”
Makamu wa Rais aliwakumbusha Viongozi hao kuhakikisha Jumuiya inashiriki kikamilifu katika kuandaa mazingira mazuri ya ushindi wa CCM katika chaguzi za Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020.
Makamu wa Rais alisema Viongozi waliochaguliwa wanajukumu kubwa la kujenga Jumuiya imara kwa kuitoa hapo ilipo na kuipeleka mbele ikiwa na kuongeza wanachama wapya kutoka katika makundi mbali mbali.
Mkutano Mkuu wa Tisa wa UWT ulifunguliwa jana na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na kufungwa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo ulifanyika uchaguzi na Mhe. Gaudensia Kabaka alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Wanawake Tanzania  na Bi. Thuwayba Kisasi alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa  Jumuiya hiyo.

No comments