Header Ads

Responsive Ads Here

BOHARI YA DAWA (MSD) MSHINDI WA PILI SEKTA ZA UMMA KATIKA TUZO YA MWAJIRI BORA 2017

 Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Bohari ya Dawa (MSD),  Victoria Elangwa (kulia), akipokea tuzo ya mshindi wa pili Sekta za Umma katika Tuzo ya Mwajiri Bora 2017 katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana.
 Wafanyakazi wa MSD wakiwa kwenye hafla hiyo.
 Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe.  Jenista Mhagama, akimkabidhi cheti cha ushiriki wa tuzo hizo  Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Bohari ya Dawa (MSD),  Victoria Elangwa. Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Anthony Mavunde.
Wafanyakazi wa MSD wakifurahia ushindi huo wakiwa na tuzo zao.

Na Dotto Mwaibale

BOHARI ya Dawa (MSD) imeibuka kidedea kwa kuwa mshindi wa  pili (2) kwa upande wa Sekta za Umma katika tuzo ya Mwajiri Bora mwaka 2017 zinazoandaliwa na Chama cha Waajiri nchini
( ATE).    

Akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo hizo, Mgeni  rasmi Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe.  Jenista Mhagama amesema uanzishwaji wa vipengele vipya katika tuzo hizo unazipa fursa za kipekee taasisi za serikali kupata nafasi ya kushiriki na  kushinda.        

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD,  Bi.Victoria Elangwa amesema tuzo hiyo ni matokeo ya maboresho ya  kiutendaji kwa MSD ambayo yanafanyika kulingana na Mpango Mkakati wa MSD wa mwaka 2017 -2020.

Ameongeza kuwa hatua hiyo ya MSD kupata tuzo ya Taasisi ya Umma inayofanya vizuri ni motisha kwa wafanyakazi na MSD kwa ujumla kufanya kazi kwa bidii zaidi.

No comments