Header Ads

Responsive Ads Here

Wanachama wa Shirikisho la waganga wa Tiba Asili Tanzania (SHIVYATIATA)wawajia juu viongozi wao


Na David John

BAADHI ya wanachama wa Shirikisho la waganga wa Tiba Asili Tanzania (SHIVYATIATA) wamewajia juu viongozi wa Shirikisho huku wakihoji uhalali wao wa kuendelea kufanya kazi.

Wamesema kuwa viongozi hao muda wao wa kuongoza ulishapita na wanachama walishatoa msimamo wa kuwataka kujiudhuru ili kupisha kufanyika kwa uchaguzi mwaka kesho.

Akizungumza kwa niaba ya wezake mmoja wa wanachama hao Rajabu Hassan amesema wamepata taarifa kwamba kuna baadhi ya viongozi wa shirikisho hilo wamekwenda mjini Dodoma kusimamia uchaguzi wa shirikisho vyama kwa ngazi ya mkoa kinyume cha taratibu.

Amesema maamuzi ya Halmashauri kuu ya shirikisho hilo ilikuwa kuwa chaguzi zote ambazo zitafanyika ngazi za wilaya na mikoa zisimamiwe na wajumbe wa halmashauri kuu na si viongozi wakuu na hiyo nikutokana wao walipewa kuendesha shirikisho kwa muda ambapo muda wao umekwisha kimsingi.

“unajuwa ndugu mwandishi kimsingi viongoza hawa hawana Sifa na kinachosubiliwa na mkutano mkuu na Hata hivyo mwenyekiti anakwenda yeye pekee yake kinyume na katiba kwani kila kitu anakwenda kufanya yeye. “Amesema Hassan

Nakuongeza kuwa pia mwenyekiti huyo amekuwa mbabe kwani ikitokea mwanachama anahoji jambo basi anatishia kumfutia uwanachama pamoja na kumuondoa kwenye makundi yao ya mawasiliano.

Naye mwanachama mwingine kwa sharti la kutotaja jina lake amesema wanajuwa mchezo unaofanyika na viongozi hao nikutaka kujitengenezea mazingira ya kuchaguliwa katika mkutano mkuu ujao uliopangwa kufanyika ndani ya shirikisho hilo mwakani.

Mmoja wa wataalamu wa Tiba hiyo ya dawa asili nchini akizungumzia hatua ya viongozi hao kuendelea kufanya kazi amesema kimsingi hadi sasa hakuna shirikisho na linasemewa mtaani tu.

” Kisheria hakuna chombo kinachoitwa shirikisho kwani uhalali wake ulishapita na hata kinachofanyika ndani ya shirikisho kwa sasa ni batili. “amesema.

Kwaupande wake Mwenyekiti wa Baraza la Tiba asili nchini Richrd Kayombo amesema mambo yanayoendelea ndani ya shirikisho hilo ni ya kwao wao kama Baraza wanafanya kazi na mganga mmoja mmoja.

Awali waliwataka watengeneze chombo kitakachowazungumzia mambo yao lakini mambo yanayofanyika wanajuwa wenyewe.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa shirikisho hilo Abdallahman Lutenga amewataka wanachama wake kutambua kuwa shirikisho ni mahala patakatifu hakuna mchwa wala nani atakayeingia hapo.

Amesem yeye anamamlaka ya kusimamia chaguzi kwani ndio rais wa shirikisho lakini ndio anaye teua na kuitisha mikutano ya shirikisho hilo.

” Nataka nikuambie kwanza wakati mwingine muwe mnauliza kwanza huko chini kabla ya kuja kwangu kwani mimi ni kiongozi mkubwa na nina kazi nyingi na anatambulika na Serikali. “amesema

Hassan Rajabu mmoja mwanachama wa shirikisho la vyama vya waganga wa tiba asili Tanzani.

No comments