Header Ads

Responsive Ads Here

Naibu Waziri Mhe Abdalla Ulega alipozindua mkakati wa Taifa wa kandomu Jijini Dar es Salaam

 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega (katikati) akikata  utepe kushiria  uzinduzi wa mkakati wa taifa wa kondomu katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam Novemba 27, 2017 kuelekea maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniania Desemba 1,2017. kulia kwake ni, Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dr, Leornad Maboko.
(PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON)
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega (katikati) akionesha  mkakati wa taifa wa kondomu mara baada ya kuzindua kuelekea maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniania Desemba 1,2017. 
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega akizungumza na wananchi mara baada ya kuzindua mkakati wa taifa kondomu kuelekea maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniania Desemba 1,2017.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dr, Leornad Maboko akieleza jinsi maambukizi ya VVU yalivyo kwa sasa.ambapo amesema takribani watu elfu 55 kwa mwaka wanamaambukizi mapya na kundi kubwa likiwa ni vijana.  kati ya hao asilimia 40 ya vijana wanamaambukizi mapya wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24.
 Mkurugenzi wa kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Neema Rusibamayira akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
 Mkurugenzi wa wa Habari na Uraghibishi Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi nchini Tanzania (TACAIDS),    Jumanne Isango akimpatia maelezo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega huhusiana na maswala ya Ukimwi alipotembelea banda hilo.
 Naibu Waziri, Abdalla Ulega akipata maelezo namna ya kuvaa kondomu ya kiume na muelimishaji kuhusu matumizi sahihi ya kondomu kutoka T- Marc Tza Benjamin Salema alipotembelea mabanda yaliyopo ndani ya Viwanja vya Mnazi leo Jijini Dar es Salaam.
 Seemu ya wananchi wakishuhudia uzinduzi wa mkakati wa kitaifa wa kandomu katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mtendaji  wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko akimuelezea jambo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega mara baada ya kusaini kitabu cha wageni.
  Naibu Waziri, Abdalla Ulega akisalimiana na Mkurugenzi wa kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Neema Rusibamayira mara baada kuwasili katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam wakati wa  kuzindua mkakati wa kitaifa wa kandomu.
 Naibu Waziri, Abdalla Ulega akisalimiana  na Mkurugenzi Mtendaji  wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko.
Naibu Waziri, Abdalla Ulega akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS,  Elizabeth Kaganda.

No comments