Header Ads

Responsive Ads Here

MAMA LISHE AMWAGIWA MAFUTA YA MOTO YA KUKAANGIA CHIPS SHINYANGA


SeeBait

Mama lishe aitwayeTeonestina Lugambwa (59) mkazi wa Majengo mjini Shinyanga, anayefanya biashara zake maeneo ya Soko la Nguzo nane mjini hapa amenusurika kifo baada ya kukabwa shingo kisha kumwagiwa mafuta ya moto yaliyokuwa yanatumika kukaangia chips na mfanyabiashara mwenzake Kulwa Ally.

Inaelezwa kuwa tukio hilo limetokea Novemba 5,majira ya saa 12 jioni katika eneo hilo la Nguzo Nane Lugambwa akitoka kununua bidhaa katika eneo hilo kwa ajiri ya maandalizi ya mauzo.

Akisimulia kuhusu tukio hilo Teonestina Lugambwa amesema chanzo cha ugomvi wao na mwenzake ni eneo la biashara ambapo chumba anachokitumia sasa awali kilikuwa kinatumiwa na mtuhumiwa lakini aliondolewa na amekuwa akilitaka kwa vile lina wateja wengi.

Ameiambia Malunde1 blog kuwa alimwagiwa mafuta hayo ya moto katika maeneo mbalimbali ya mwili wake ikiwemo kwenye mikono,begani,mgongoni na usoni.

Kaimu Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga Lutusyo Mwakyusa amesema tayari wanamshikilia mtuhumiwa na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.
Teonestina Lugambwa akionesha majeraha yaliyotokana na kumwagiwa mafuta ya moto ya kukaangia chips-Picha na Marco Maduhu - Malunde1 blog
Majeraha ya mafuta ya moto kwenye mikono
Teonestina Lugambwa  akionesha majeraha

Picha na Marco Maduhu - Malunde1 blog

No comments