Header Ads

Responsive Ads Here

CHUO CHA KODI KUFANYA MAHAFALI YA KUMI JUMAMOSI NOVEMBA 18 2017


Chuo cha Kodi kitafanya mahafali ya Kumi Jumamosi tarehe 18 Novemba 2017 katika ukumbi wa chuo cha Kodi ambapo Mgeni rasmi katika mahafali hayo anatarajiwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.

Katika mahafali hayo, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mpango atatunuku vyeti, stashahada na shahada kwa wahitimu 520 ambao wamefuzu masomo yao mwaka 2016/2017 na kusathili kutunukiwa vyeti.

Dkt. Mpango pia atatoa zawadi mbalimbali kwa wahitimu 12 waliofanya vizuri zaidi katika masomo ikiwa ni utaratibu ambao chuo kimejiwekea ili kutambua jitihada nzuri ambazo zimefanywa na wanafunzi hao pamoja na kuwashajihisha wanafunzi wanaoendelea na masomo kufanya vizuri zaidi katika masomo. 

Jumla ya anafunzi watakao tunukiwa vyeti, stashahada na shahada katika mahafali ya Kumi ya Chuo cha Kodi ni wahitimu 82 wa Cheti cha Uwakala wa Forodha cha Afrika Mashariki yaani the ‘East African Customs and Freight Forwarding Practising Certificate (EACFFPC). Wahitimu 39 wa Cheti cha Usimamizi wa Forodha na Kodi yaani ‘Basic Technician Certificate in Customs and Tax Management (CCTM). Stashahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi yaani ‘Diploma in Customs and Tax Management – (DCTM)’ wahitimu – 147, Shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi yaani ‘Bachelor of Customs and Tax Management (BCTM)’ Wahitimu – 134, ‘East African Community Postgraduate Certificate in Customs Administration (PGCCA)’ wahitimu 85 na Stashahada ya Uzamili katika Kodi yaani ‘Postgraduate Diploma in Taxation (PGDT) wahitimu - 33

Pamoja na kutunuku vyeti stashahada, na shahada kwa wahitimu, Mgeni Rasmi pia atatoa tuzo kwa wahadhiri wa Chuo cha Kodi waliofanya tafiti mbalimbali katika kipindi cha mwaka wa masomo wa 2016/2017 na kuchapishwa katika majarida mbalimbali ya kitaaluma, ikiwa ni pamoja na jarida la Chuo cha Kodi yaani ‘Journal of the Institute of Tax Administration’ (JITA).

Vilevile Chuo cha Kodi kinasherehekea miaka kumi tangu kipate ithibati (usajili) kutoka Baraza la Taifa la Vyuo vya Ufundi (NACTE).Chuo cha Kodi kinajivunia miaka kumi ya mafanikio katika kutoa mafunzo ya Forodha na Kodi yanayokidhi soko la ajira katika nyanja za forodha na Kodi ndani na nje ya nchi.

Tangu kipate usajili wa kudumu kutoka Baraza la Vyuo vya Ufundi (NACTE), Chuo kimepanua wigo wa taaluma kutoka kutoa mafunzo kwa watumishi wa TRA pekee hadi kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa masuala ya forodha na kodi kwa nchi za Mashariki Kati na Kusini mwa Afrika. 

Kikiwa katika hatua za mwisho za utekelezaji wa Mkakati wa Tatu, Chuo cha Kodi kinaendelea na maandalizi ya kuwa Kituo cha Umahiri wa Forodha na Kodi katika Ukanda wa Afrika Mashariki baada ya Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kukiteua Chuo cha Kodi kuwa Kituo cha Umahiri Afrika Mashariki

Nachukua fursa hii kuwakaribisha wahitimu pamoja wageni waalikwa wote pamoja na nyinyi waandishi wa habari katika mahafali haya ya Kumi yatakayofanyika katika Ukumbi wa Multipurpose Chuo cha Kodi tarehe 18 Novemba 2017 kuanzia saa tatu asubuhi.

“Pamoja Tunajenga Taifa Letu”
Prof. Isaya J. Jairo
MKUU WA CHUO


Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA,) Profesa Isaya Jairo akiongea na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu mahafali ya kumi ya chuo hicho yanayotarajiwa kufanyika chuoni hapo Jumamosi Novemba 18 2017. Kushoto ni Afisa Uhusiano Mkuu wa chuo, Oliver Njunwa. (Picha na Robert Okanda wa Okanda blogs) 
Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) Profesa Isaya Jairo akiongea na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu mahafali ya kumi ya chuo hicho yanayotarajiwa kufanyika chuoni hapo Jumamosi Novemba 18 2017. Kulia ni Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo (Utawala), Emmanuel Masalu na Afisa Uhusiano Mkuu wa chuo, Oliver Njunwa.

No comments