Header Ads

Responsive Ads Here

BENKI YA KILIMO YATEMBELEA ENEO LA MRADI LA UMWAGILIAJI LA MWAMANYILI WILAYANI BUSEGA


 Mkuu wa wilaya ya Busega, Tano Seif Mwera (kulia) akiwakaribisha wageni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania waliofika kijijini Mwamanyili kujionea chanzo cha maji na eneo litakalotumika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji. Wageni hao waliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila (kushoto).
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Njiginya (mbele kulia) akiwaongeza wageni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania kujionea chanzo cha maji kitakachotumika katika mradi wa umwagiliaji wa Mwamanyili.
 Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Eng. Tumbu akitoa maelekezo kwa ugeni kutoka TADB juu ya chanzo cha maji cha maji kitakachotumika katika mradi wa umwagiliaji wa Mwamanyili.
 Muonekano wa eneo likalotumika kwa ajili ya mradi wa kilimo umwagiliaji wa Mwamanyili.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (aliyenyanyua mikono) akihimiza jambo wakati walipotembelea eneo likalotumika kwa ajili ya mradi wa kilimo umwagiliaji wa Mwamanyili.

Katika kutekeleza kwa vitendo maagizo ya serikali ya kuchochea mapinduzi ya kilimo, Bodi ya wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imetembelea eneo utakaofanyika mradi wa kilimo cha kisasa cha  umwagiliaji la Mwamanyili Wilayani Busega mkoani Simiyu.

Akizungumza lengo la ziara hiyo, mkuu wa msafara huo ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila amesema lengo kubwa la kuanzishwa kwa Benki ya Kilimo ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwakwamua wakulima nchini kutoka katika kilimo cha kujikimu na kwenda kwenye kilimo cha kibiashara ili waweze kujiongezea kipato.

Aliongeza kuwa Mradi huo wa kilimo cha umwagiliaji ukianza kufanya kazi utatimiza malengo hayo ya Benki kwani utasaidia kwa kiwango kikubwa katika kuwainua wananchi Kiuchumi na kukabiliana na upungufu wa chakula wakulima watakaolima katika skimu hiyo.

“Benki ya Kilimo ipo tayari kuunga mkono miradi ya aina hii ambayo inalenga katika kuendeleza miundombinu muhimu ikiwemo ya uendelezaji wa skimu za umwagiliaji, usafirishaji, hifadhi ya mazao, usindikaji, pamoja na masoko ili kumuongezea mkulima kipato,” alisema.

Kwa mujibu wa mapendekezo ya mradi huo ambao unajumuisha zaidi ya ekari 2050, wananchi watakaolima katika skimu hiyo watazalisha mpunga kwa misimu miwili kwa mwaka na kupanda mazao mengine mbadala hususani ya jamii ya mikunde mara baada ya kuvuna mpunga, kwa ajili ya kurutubisha ardhi.

No comments