Header Ads

Responsive Ads Here

YANGA YAISHUSHA KILELENI SIMBA ‘YAIDUNGUA KAGERA SUGAR’ VIWANJA VINNE NGOMA MBICHI


Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Yanga kwa mara ya kwanza leo wamepata ushindi wa zaidi ya goli moja baada ya kuifunga 2-1 Kagera Sugar kwenye mchezo wa VPL uliochezwa uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Yanga walikuwa hawajapata ushindi uliozidi goli moja kwenye ligi katika mechi zao tano zilizopita.
Ushindi dhidi ya Kagera umeipa Yanga pointi tatu na hatimaye wamefikisha pointi 12 baada ya kucheza mechi zao sita za ligi. Yanga inapanda kwenye msimamo kutoka nafasi ya sita hadi ya kwanza ikiwa sawa kwa pointi na Azam ambayo imelezimishwa sare ya kufungana 1-1 Mwadui huku Yanga na Azam zikisubiri matokeo ya kesho ya Simba dhidi ya Mtibwa.
Simba wapo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 11 pointi moja nyuma ya Yanga na Azam, Simba wanasubiri kucheza kesho dhidi ya Mtibwa ili kufikisha mechi sita. Endapo wakishinda watafikisha pointi 14 na kurejea kwenye nafasi ya kwanza, wakitoka sare watakuwa na pointi 12 sawa na Yanga na Azam lakini Simba ina idadi nzuri ya wastani wa magoli hivyo bado itaendelea kuongoza ligi.
Mtibwa pia ina nafasi nzuri ya kuongoza ligi endapo itashinda mchezo wa kesho dhidi ya Simba, Mtibwa ina pointi 11 sawa na Simba na Singida United (tayari Singida imecheza mechi sita) Mtibwa nayo ikipata sare itafikisha pointi 12 sawa na Yanga na Azam.
Matokeo ya mechi nyingine za leo
  • Ruvu Shooting 0-0 Singida United
  • Mwadui 1-1 Azam
  • Ndanda 1-1 Majimaji
  • Njombe Mji 0-0 Lipuli

No comments