Header Ads

Responsive Ads Here

WILAYA YA BIHARAMULO YACHAGULIWA KUWA KITOVU CHA KUZALISHA ZAO LA MHOGO MKOANI KAGERA

 Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mwaluka (mwenye koti jeusi), akipanda mche wa kwanza wa Mhogo  kwenye shamba darasa katika Kijiji cha Besheshe wilayani humo mkoani Kagera wakati akizindua shamba darasa hilo na upandaji mbegu bora ya mhogo leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya hiyo, Wales Mashanda.
 Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karagwe, Dauson Byamanyirwohi akizungumzia soko la mhogo katika wilaya hiyo.
 Wakulima wakiandaa shamba darasa katika Kijiji cha Bisheshe. 

 Mtafiti kutoka OFAB. Dk. Beatrice Lyimo akizungumza kwenye uzinduzi wa shamba darasa katika Kijiji cha Bisheshe.
 Kaimu Mkurugenzi wa wilaya hiyo, Ashura Kajuna, akizungumza.
 Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya hiyo, Wales Mashanda, akizungumza.
 Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mwaluka, akitoa hutuba ya uzinduzi wa shamba darasa la mbegu ya mhogo katika Kijiji cha Kisheshe.
 Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo ARI- Maruku kilichopo mkoani Kagera Jasmeck Kilangi akitoa elimu kwa wananch,wakulima na viongozi juu  ya kilimo bora cha zao la Muhogo wakati wa uzinduzi wa upandaji wa shamba darasa la mihogo kwenye Kijiji cha Kisheshe.
  Kaimu Mkurugenzi wa wilaya hiyo, Ashura Kajuna na Ofisa Kilimo wa wilaya hiyo wakishiriki kupanda mbegu ya mhogo.
Shamba darasa likiandaliwa katika Kata ya Rugera Kijiji cha Nyalugando.

Na Dotto Mwaibale, Karagwe, Kagera

WILAYA ya Biharamulo mkoani Kagera imechaguliwa kuwa kitovu cha kilimo cha zao la mhogo mkoani humo ili kuwainua wananchi kiuchumi.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karagwe, Dauson Byamanyirwohi wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Rugera mkoani Kagera jana wakati wa uandaaji wa shamba darasa la mbegu ya mihogo katika kata hiyo.

Byamanyirwohi amewahakikishia wakulima hao kuwa kwa sasa soko la Muhogo ni kubwa sana baada ya serikali ya Tanzania kusaini mikataba na serikali ya china kwa ajili ya kuiuzia nchi hiyo mihogo hivyo wazalishe kwa wingi ili wajipatie kipato cha kutosha.

Alisema Mkoa wa Kagera umeiteua wilaya ya Biharamulo kuwa ndiyo itakuwa kitovu cha uzalishaji wa zao la muhogo na kujenga kiwanda kikubwa cha kuchakata zao hilo hali ambayo itawarahisishia wanakulima wa zao hilo mkoani Kagera kuacha kwenda kuuza mihogo yao kwenye soko la Uganda.

Kauli hiyo ilikuja baada ya baadhi ya wananchi kuuliza uhakika wa soko la muhogo kutokana na zao hilo kustawi sana kwenye kijiji chao na hasa baada ya kupewa mbegu hizo bora ambazo zina zaa sana na hazishambuliwi na magonjwa makubwa ya mihogo ambayo yanapunguza uzalishaji wa zao hilo kijijini hapo.


Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mwaluka amesema kuwa kamwe hakutakuwa na Tanzania ya viwanda endapo wakulima hawataweza kuingia mashambani na kuzalisha mazaodfrey Mwaluka o ya kutosha kulisha viwanda hivyo ambavyo serikali ya awamu ya tano inahimiza na kuhamasisha vijengwe nchi nzima.

Mwaluka aliyasema hayo wakati akizungumza na wakulima  kabla ya kuzindua shamba darasa la Mihogo na mbegu kwenye Kijiji cha Bisheshe wilayani humo  kupitia program ya kuwawezesha wakulima wa wilaya hiyo kulima kisasa na kwa kutumia mbegu bora inayoendeshwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB).

Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wananchi hao kutambua kuwa mpango huo wa serikali ya awamu ya tano unawategemea sana wakulima hivyo kabla viwanda vya kuchakata mihogo havijajengwa lazima malighafi iwepo ili wawekezaji waweze kuwa na uhakika na upatikanaji wa mali ghafi mbalimbali.

“Hakikisheni  mbegu hizi bora za mihogo mnazopewa mnazitunza  ili kutoa nafasi kwa wananchi wengi zaidi kujifunza mbinu bora za kilimo hiki kupitia shamba darasa hili ili kila mkazi wa Karagwe aweze kulima na kuzalisha kwa tija” Alisisitiza Mkuu wa wilaya ya Karagwe Mhe. Mwaluka.

Hata hivyo Mwaluka ameishukuru COSTECH kwa kuamua kuipatia wilaya hiyo mashamba darasa mawili ya mazao ya muhogo kwani anaamini mbegu hizo zitasimamiwa vizuri na kasha kuwafikia wakulima wengi zaidi kwenye wilaya hiyo ili waweze kuachana na mbegu zao za zamani ambazo zinashambuliwa sana na magonjwa ya batobato kali na michirizi ya kahawia.

Kaimu Mkurugenzi wa wilaya hiyo, Ashura Kajuna alisema kuwa kwa muda mrefu wilaya ya Karagwe na Mkoa wa Kagera wananchi wake wamejikuta wakikumbwa na changamoto ya ukosefu wa chakula kutokana na chakula chao kikuu kwa maana ya Migomba kukumbwa na ugonjwa hatari wa Mnyauko na hivyo kuathiri sana uzalishaji wa zao hilo.

Alisema ujio wa mbegu hizo bora za mihogo ambazo zina ukinzani na magonjwa ya batobato kali na michirizi ya kahawia ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa wilaya hiyo na mkoa kwa ujumla kwani unawahakikishia usalama wa chakula tofauti na hapo awali ambapo walitegemea zao la muhogo pekee.

Kaimu Mkurugenzi huyo aliahidi kushirikiana na wataalamu kutoka COSTECH na Kituo cha utafiti wa kilimo Maruku katika kusimamia program hiyo na mashamba hayo ili wananchi waweze kufaidi matunda ya mbegu hizo bora ambazo zimefanyiwa utafiti na kuwanufaisha wananchi wa mikoa mbalimbali nchini ambao wameshatumia mbegu hizo.

Akieleza lengo la COSTECH na OFAB kuendesha program hiyo mkoani, Kagera Mtafiti kutoka OFAB, Dk. Beatrice Lyimo alisema kuwa kazi ya COSTECH ni kuhakikisha matunda ya kazi nzuri za tafiti yanawafikia wakulima na wananchi wengine kwenye Nyanja mbalimbali hivyo hii ni moja ya utekelezaji wa majukumu ya tume hiyo.

Alisema kwa miaka mingi tafiti mbalimbali nzuri zimekuwa zikifanywa na watafiti hapa nchini lakini haziwafikii walengwa akitolea mfano wakulima,lakini COSTECH ikatafuta fedha na kuitoa tafiti hiyo kwenye vituo vya utafiti na kuwapelekea wakulima ili kusaidia kutatua changamoto ambazo zinawakabilia kwenye kilimo chao.

Dk. Lyimo aliwataka wakulima hao kuhakikisha wanashirkiana na maofisa ugani kwenye vijiji vyao,kata na wilaya katika kuhakikisha shamba darasa hilo linakua na kusaidia kutoa elimu kwa wananchi wengine lakini pia kuzaiisha mbegu za kutosha kwaajili ya mashamba yao na wananchi wengine wa wilaya hiyo.

Ofisa Kilimo Mkoa wa Kagera, Louis  Baraka amewataka  wataalamu wa kilimo kwenye mkoa huo kuhakikisha wanawafundisha wananchi kulima na kutunza chakula cha kutosha mwaka mzima kwa matumizi ya familia zao badala ya kuuza chakula chote mara baada ya kuvuna na kuanza kununua chakula.

“kumekuwa na tabia wananchi wanavuna maharage mengi sana au mahindi lakini miezi michache baada ya kuvuna unaona wanakwenda kunua maharage hayohayo kwa wakulima wenzao au madukani kwa bei kubwa kitu ambacho sio kizuri kabisa na kinachochea kuwepo kwa njaa kusiko kwa lazima kwenye kaya” alisema Baraka.

Zoezi hilo la uanzishwaji wa mashamba darasa ya mbegu bora za Mihogo,Viazi lishe na Migomba iliyozalishwa kwa njia ya chupa linajumuisha wilaya Tano za Mkoa wa Kagera mara baada ya COSTECH na OFAB kutoa mafunzo kwa wataalamu wa kilimo wa iwlaya zote kutoka kata zote ili kuweza kusimamia vizuri ili kuwasaidia wakulima kuzalisha kwa tija na kuachna na kilimo chao cha mazoea.No comments