Header Ads

Responsive Ads Here

WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI WAZIRI MASAUNI AWATAKA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO KUVIFANYIA UKAGUZI, MAKAMPUNI KADHAA YADHAMINI


2
Naibu waziri wa Ujenzi Mh. Elias Kwandikwa akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo uliozungumzia maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa usalama Barabarani  umefanyika kwenye makao  makuu  ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi leo , Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Yusuf Masuni.

IMG_8324
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Yusuf Masuni akifafanua jambo katika mkutano huo uliofanyika leo.
IMG_8338
Naibu Waziri wa Ujenzi Mh. Elias Kwandikwa akimkabidhi cheti cha kumtambua msanii wa ngoma za asili Mrisho Mpoto kutokana na mchango wake katika kupunguza ajali kwa kutoa elimu ya Usalama Barabarani. wa pili kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Yusuf Masauni.
IMG_8339
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Yusuf Masauni na Naibu Waziri wa Ujenzi Mh. Elias Kwandikwa  wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii mara baada ya kuwakabidhi vyeti vyao.
…………………………………………………………………………………..
Zikiwa Zimebaki Siku Chache Kuelekea Wiki Ya Nenda Kw Ausalama Barabarani Wamiliki Na  Madereva Wa Vyombo Vya Usafirishaji Nchini wametakiwa   Kukagua Vyombo Vyao Vya Usafirishaji Mapema  Ili Kubaini Matatizo Mbalimbali Ya Vyombo Hivyo Na Kuvifanyia Marekebisho Ili Kuepuka  Usumbufu Juu Yao
  Agizo Hilo Limetolewa Leo Na Mh Yusufu Masauni Naibu Waziri Wa Mambo Ya Ndani ya Nchi Alipokuwa Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Ofisini Kwake Na Kuwataka Wamiliki Na Madereva Wa Vyombo Vya Usafiri Kutii  Sheria Bila Shurti Kwani Adhabu Kali Zitachukuliwa Juu Yao na Baada Ya Ukaguzi magari yao Yatabandikwa Stika Maalum Ili Kuwabaini Watakaokaidi Agizo Hilo
Aidha Mh Masauni Amebainisha kuwa Magari Ambayo Yanatakiwa Kufanyiwa Ukaguzi Mapema Ni Magari Ya Wanafunzi Magari Ya Kubeba Mizigo Na Mabasi Ya Abiria Pia Amewataja Mawakala Ambao Watashirikiana Nao Kuyafanyia Uchunguzi Magari Hayo Ni Temesa Pamoja Na NIT Maadhimisho Hayo Kwa Mwaka Huu Kitaifa Yatafanyika Mkoa Kilimanjaro Yatazinduliwa Rasmi Tarehe 16/10/2017 Hadi Tarehe21/10/2017 Katika Viwanja Vya Shujaa Na Mgeni Rasmi Atakuwa Ni Makamu Wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan, “Kauli Mbiu Ya Mwaka Huu Ni Zuia Ajali Tii Sheria Okoa Maisha”
Hata Hivyo Mh Masuni Ameyashukuru Makampuni Mbalimbali  Ikiwemo Vodacom Geita Gold Mine Selcom, Vodacom na Puma. Na TBL Kwa Kufanikisha Maadhimisho Hayo Kwa Kutoa Ushirikiano Wa Hali Na Mali,
Akizungumza Katika Kikao Hicho Afisa Mawasiliano wa Mambo Ya Nje  TBL Amanda Walter Amesema Wamekuwa Wakishiriki Kwa Miaka 9 katika Kampeni Mbalimbali Za Usalama Barabarani  Hivyo  Kampuni  Hiyo Kwa Mwaka Huu  Imejitolea Milioni Thelathini Kwa Ajili Ya Kuwapima Afya  Madereva 1000 Magonjwa Mbalimbali  Ikiwemo Macho, Maralia Na Kisukari
Nae Bwana  Shayo kutoka Kampuni ya mgodi wa Geita Gold Mine Amesema  Kampuni Yao Imetoa Shilingi Milioni Sitini Na Mbili Kwa Ajili Ya Stika Hizo Ili Kukamilisha Maadhimisho hyo Pia Amesema Wameamua Hivyo Kwakua Usalama Barabarani  Ni Wa Kila Mmoja Hayabagui Mtu

No comments