Header Ads

Responsive Ads Here

WAZIRI UMMY ATOA MIEZI SITA KUANZISHA MADAWATI YA ULINZI NA USALAMA WA WATOTO SHULENI


Pix 1
1Waziri wa Afya, Maendeleo  ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy  Mwalimu akizungumza na wananchi wa Tarime mkoani Mara na kutoa miezi sita kwa wakuu wa shule za Msingi na Sekondari kuanzisha madawati ya ulinzi na usalama kwa mtoto kike katika Shule zao.

Pix 2
Mkuu Wa mkoa wa Mara Mhe. Charles Mlingwa  akihamasisha wananchi wa mkoa wa Mara kuzingatia na kulinda haki za Mtoto katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike iliyofikia kilele chake 11/10/2017.
Pix 3
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,  Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizindua kampeni ya kitaifa ya kutokomeza mimba za utotoni yenye kauli mbiu isemayo:” “Najitambua Elimu ndio Mpango mzima”.
Pix 4
Waziri wa Afya,  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akibonyeza kitufe kuzindua ujumbe wa radio wa kampeni ya kutokomeza mimba za utotoni yenye kauli mbiu isemayo:” Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima”
Pix 5
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto, wadau na madereva bodaboda wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara muda mfupi baada ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika kitaifa wilayani Tarime mkoani Mara.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
……………..
Na Mwandishi Wetu Tarime- Mara.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ametoa miezi sita kwa Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari nchini kuanzisha Madawati ya Ulinzi na Usalama wa Watoto kwa ajili ya kusikilizamatatizo ya wanafunzi hasa wanafunzi wa kike.
Akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa KikeKitaifa iliyofanyika katika wilaya ya Tarime mkoani Maraamewasisitiza wakuu wa shule za Msingi na Sekondari kuzingatia uwepo wa dawati la ulinzi na usalama wa mtoto  kike katika shule zao ili kuwa salama na kuwa na mahali pa keleza matatizo yao.
Mhe. Ummy ameongeza kuwa suala la kumlinda mtoto wa kike ni jukumu la kila moja katika jamii na kuwapongeza wadau wa maendeleo ya watoto kwa jitihada zao na kushirikiana na Serikali kutoa elimu kwa wanajamii kuhusu madhara ya mimba za utotoni, ukeketaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
“ Niwatake wakuuwashule za msingi na Sekondari kuanzisha madawati kwa ajili ya ulinzi na usalama wa  watoto wa kike kwa ajili ya kusikiliza shida za wanafunzi wa kike na kuwasaidia kutatua shida zao katika ngazi ya shule”.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la kutokomeza ukeketaji Tarime Stela Mgaya amesema kuwa wamefanikisha kuwaondoa mangariba 63 kutokakatika kazi ya ungariba na kuwatafutia kazi zingine za kujipatia kipato.
Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Watoto Duniani UNICEF Bi. Maniza Zaman amewasihi viongozi wa dini na wale wa Kimila ambao  wana ushawishi mkubwa kuziongoza jamii zetu kuwaangalia na kuwasaidia watoto wa Kike.
Mwakilishi Shirika la Plan Tanzania Bi. Martha Lazaro ameishukuru Serikali na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiao katika kutekeleza mipango mbalimbali ya mtoto hasa wa kike na vihatarishi vinavyopelekea kuharibu maisha yao.
Katika Maadhimisho ya mwaka huu Serikali imezindua Kampeni ya Kitaifa ya utokomezaMimba za Utotoni yenye kauli mbiu isemayo:“ Tutokomeze Mimba za Utotoni; Tufikie Uchumi wa Viwanda”. Maadhimidho hayo, Waziri Ummy ameteua wimbo wa Shule ya Sekondari ya Welwel na Karatu zote za wilayani Karatu, Arusha kuwa wimbo mahususiutakaotumika kuhamasisha na kuelimisha jamii kutokomeza mimba za utotini.

No comments