Header Ads

Responsive Ads Here

WAZIRI MAKAMBA ATEMBELEA OFISI ZA URATIBU ZA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR


DSC_4780
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiwa katika kikao wa watumishi wa Ofisi ya Uratibu – Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Waziri Makamba amepata wasaa wa kuzungumza na Menejimenti na watumishi wa Ofisi hiyo leo jijini Dar es Salaam, Mtaa wa Luthuli.

DSC_4798
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Uratibu – Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri January Makamba mara baada ya kutembea Ofisi zao zilizopo Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam.
……………..
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba hii leo amefanya ziara ya kikazi kutembelea Ofisi za Uratibu wa shughuli za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) zilizopo Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam.
Katika Ziara hiyo Mhe. Makamba amepata fursa ya kuongea na Menejimenti ya Ofisi hiyo na kupata wasaa wa kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya kuimarisha ushirikiano zaidi baina yao.
Awali, akimkaribisha Waziri Makamba, Mratibu Mkuu Bw. Issa Mlingoti amemshukuru Waziri Makamba kwa kufika na kuahidi kuimarisha ushirikiano katika nyanja za Elimu, ajira na fursa kwa pande zote za Muungano.
“Sisi tumefarijika sana kwa ujio wako na tunategemea kuwa huu ni mwanzo na mwelekeo mzuri wa kuzidi kuimarisha mashirikiano baina yetu ikiwa sisi ni waratibu wa shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar” Alisisitiza Bw.Mlingoti
Katika ziara hiyo Waziri Makamba alipata fursa ya kuongea na wafanyakazi, kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuahidi kuzipatia ufumbuzi.

No comments