Header Ads

Responsive Ads Here

WAZIRI KAMWELWE AKAGUA MIRADI YA MAJI KISARAWE


1Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Inj. Romanus Mwag’ingo akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji inayotegemewa kutekelezwa na DAWASA katika Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani.

2Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Isack Kamwelwe akitoa maagizo kwa viongozi na watendaji wa Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maji.
3Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Isack Kamwelwe akiwa mbele ya Bwawa la Maji la Chole Semvula alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maji katika Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani.
4Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Isack Kamwelwe akiwa kwenye mradi wa maji wa Mengwa pamoja na viongozi na watendaji wa Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maji.
…………….
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Isack Kamwelwe amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Kisarawe, mkoa wa Pwani kufuatilia maendeleo ya Sekta ya Maji katika wilaya hiyo.
Dhumuni la ziara hiyo ilikua ni kukagua utekelezaji ya miradi ya maji inayotekelezwa na serikali katika wilaya hiyo, yenye changamoto kubwa ya huduma ya maji licha ya kuwa ni moja ya miji ya muda mrefu na historia kubwa nchini.
“Nimetembelea wilaya kadhaa za mkoa Pwani zikiwemo Rufiji, Mkuranga na Kibiti, lakini hapa Kisarawe kuna changamoto kubwa. Inabidi tufanye kazi ya ziada ili kuinua kiwango cha huduma ya maji ambacho ni asilimia 46, naagiza viongozi wa wilaya mje ofisini kwangu Dodoma tuweke mikakati ya kuinua hali ya maji Kisarawe”, alisema Inj. Kamwelwe.
Inj. Kamwelwe alisema kuwa anamshukuru Mhe. Rais kwa kuagiza DAWASA waje Kisarawe, kwa kuwa watasaidia kuinua kiwango cha huduma ya maji kwa wakazi wa Kisarawe. DAWASA watatoa maji Ruvu Juu na baada ya miezi 15 maji yatakuwa yamefika Kisarawe.
Aidha, Waziri wa Maji na Umwagiliaji alitembelea miradi ya maji ya Mengwa, Kikwete na bwawa la maji la Chole Semvula lilioanza utekelezaji wake mwaka 2013 ambalo utekelezaji wake ulikuwa umesimama kwa changamoto mbalimbali, na kusema kuwa ni bwawa zuri, lililo katika mazingira mazuri na lina maji na kuagiza kuanza utekelezaji wake mara moja.

No comments