Header Ads

Responsive Ads Here

WAZIRI KALEMANI AMKABIDHI OFISI WAZIRI WA MADINI ANGELLAH KAIRUKI


1
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani akimkabidhi Ofisi Waziri wa Madini, Angellah Kairuki. Wanaoshuhudia katikati ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, kulia kwaDkt. Kalemani ni Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu na wa kwanza kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Prof. James Mdoe.


3
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani (katikati mbele), Waziri wa Madini Angellah Kairuki (katikati mbele), Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu (kushoto) Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (Kushoto kwa Waziri Angellah Naibu Waziri wa Nishati, Katibu Mkuu Prof. James Mdoe wakifuatilia kikao kati ya viongozi hao na Wajumbe wa Menejimenti wa iliyokua Wizara ya Nishati na Madini.
2
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani (kulia aliyekaa) Waziri wa Madini Angellah Kairuki kushoto(aliyekaa) wakiweka saini Nyaraka za Makabidhiano ya Wizara. Wanaoshuhudia ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo , Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na Kaimu Katibu Mkuu Prof. James Mdoe (wa kushoto
4
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (aliyesimama) akieleza jambo wakati wa kikao kati ya vingozi hao na Menejimenti ya iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini
…………..
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani amemkabidhi Ofisi Waziri wa Madini, Angellah Kairuki. Walioshuhudia Makabidhiano hayo ni Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, Naibu Waziri Wa Madini, Stanslaus Nyongo, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara za Nishati na Madini, Prof. James Mdoe na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo.
Vilevile, Dkt. Kalemani ametumia fursa hiyo kuwaaga na kuwashukuru kwa ushirikiano waliompa waliokuwa Watumishi wa iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Dkt. Kalemani amempongeza Kairuki kwa kuchaguliwa kwake kuwa Waziri wa kwanza Mwanamke wa Wizara ya Madini na kumweleza kuwa, Watanzania wana matumaini makubwa na mabadiliko ya Wizara na kuongeza kuwa, pamoja na majukumu mengine analo jukumu la kuhakikisha anaendeleza mikakati ya Serikali ya kuendeleza uanzishwaji migodi mipya hususan ya madini ya viwandani kama Graphite.
Naye Waziri Kairuki amesisitiza suala la ushirikiano kwa watumishi wa Wizara husika ili hatimaye kuwezesha sekta husika kuwa na mchango zaidi kwa taifa na  hatimaye watanzania waweze kunufaika zaidi na Rasilimali hiyo.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amesema kuwa viongozi wa wizara husika wanao wajibu wa kuonesha mchango wa madini katika pato la Taifa hivyo amesisitiza uwepo wa ushirikiano kati ya Viongozi na Watumishi wa Wizara ili wajibu huo utekelezwe

No comments