Header Ads

Responsive Ads Here

WAZIRI KAIRUKI AKUTANA NA WATENDAJI WA WIZARA, TAASISI NA MIRADI

Picha Na 1
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (mbele) akiongoza kikao kilichoshirikisha  watendaji wa  Wizara, Taasisi na miradi iliyo chini yake kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam
Picha Na 2
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki akitoa maelekezo kwa watendaji wa Wizara, Taasisi na miradi iliyo chini yake (hawapo pichani)
Picha Na 3Picha Na 4
Sehemu ya watendaji wa Wizara ya Madini, Taasisi na miradi iliyo chini yake wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri  wa Madini, Angellah Kairuki (hayupo pichani)
Picha Na 5
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akifafanua jambo katika kikao hicho.
Picha Na 6
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kushoto) na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Kamishna wa Madini Nchini Mhandisi Benjamin Mchwampaka (hayupo pichani) katika kikao hicho.
Picha Na 7
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Mhandisi John Nayopa akitoa ufafanuzi katika kikao hicho.
Picha Na 8
Kamishna wa Madini Nchini Mhandisi Benjamin Mchwampaka akielezea sekta ya madini katika kikao hicho.
…………..
Waziri  wa Madini, Angellah Kairuki  leo tarehe 21 Oktoba, 2017 amekutana na watendaji wa Wizara pamoja na  Taasisi na Miradi  katika Ofisi za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kujadili mafanikio na changamoto za miradi ya maendeleo. Taasisi na miradi iliyoshiriki ni pamoja na  Shirika la Madini la  Taifa (STAMICO), Mradi wa Usimamizi  Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) na Mpango wa Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya  Uziduaji (TEITI). Kikao hicho pia  kilishirikisha Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo

No comments