Header Ads

Responsive Ads Here

WATAALAM : KULAZA WATOTO WACHANGA CHALI HUPUNGUZA VIFO VYA GHAFLA


SeeBait
Akinamama wameshauriwa kuzingatia kuwalaza watoto wao kwa mgongo yaani chali na sio kifudifudi kama ilivyozoeleka kwa wanawake wengi ili kupunguza hatari ya matatizo ya vifo vya ghafla vya watoto yaani Sudden Infant Death Syndrome ‘SIDS’.

Kufuatia taarifa iliyo ripotiwa na CNN kuhusu suala hili siku za karibuni, inashauriwa kuwa watoto walio na umri wa chini ya mwaka mmoja ni vizuri wakalazwa chali kwani wako kwenye hatari ya kukosa hewa vizuri au kupaliwa pindi wanapokua wamelazwa kifudifudi na wakapoteza maisha.

Imeripotiwa kuwa kwa mwaka 2015 zaidi ya watoto 1600 nchini Marekani walikufa vifo vya ghafla kwasababu kulazwa kwa namna hiyo.

No comments